Ester Bulaya Achafua Hali ya Hewa Bungeni Baada ya Kumfananisha Waziri Maghembe na TISHU

Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya jana alichafua hali ya hewa bungeni baada ya kusema kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ni mzigo na mwepesi kama ‘tishu’ kwa sababu hana uwezo wa kusimamia mambo mazito yaliyopo katika wizara hiyo, kama vile migogoro ya wananchi na hifadhi za Taifa.

“Huyu waziri ni mzigo kama alivyowahi kusema (Abdulrahman) Kinana. Mimi nasema yeye ni mwepesi kama tishu, hawezi kuisaidia wizara hii nyeti,” alisema mbunge huyo jana wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama alisimama na kuomba mwongozo wa mwenyekiti juu ya mbunge huyo kutumia maneno ya kuudhi ambao uliungwa mkono na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge aliyemtaka Bulaya kufuta neno mwepesi kisha aendelee na hotuba yake. Hata hivyo, Bulaya alikataa kufuta neno hilo na kusema wabunge hawaamuliwi maneno ya kutumia.

Chenge aliendelea kumsihi mbunge huyo kufuta neno hilo na katika mabishano hayo yaliyodumu kwa dakika tatu, baadaye, Bulaya alikubali kuondoa neno ‘tishu’ na kuliacha neno mwepesi na kuruhusiwa kuendelea kuchangia.

“Mwenyekiti sitafuta neno mwepesi, kama neno ‘tishu’ linawakera basi naliondoa libaki mwepesi,” alisema Bulaya.

Katika mchango wake, Bulaya alisema wananchi wanaoishi katika hifadhi zilizopo jimboni mwake wananyanyaswa na askari wanyamapori wakati Serikali imeshindwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya kuishi.

Alimtaka waziri huyo kushughulikia kero zote zinazowakabili wananchi wa Bunda akisema Serikali haiendeshwi kwa maneno matupu, bali vitendo na dhamira ya dhati ya kuwahudumia wananchi.

“Tatua matatizo jimboni kwangu ili niweze kukupima kama wewe ni mzito au mwepesi,” alisema mbunge huyo akimwambia Profesa Maghembe.

Baada ya Bulaya kumaliza muda wake, mbunge aliyefuatia alikuwa Abdallah Ulega wa Mkuranga (CCM) ambaye alisema kuna haja ya wabunge kupimwa kama wamelewa getini ili kujua akili zao.

“Kijana aliyefunzwa vizuri hawezi kumtukana mzee kama yule (Maghembe). Kama suala ni uwaziri basi aangalie hata umri wake kabla ya kuzungumza... Naungana na aliyesema wabunge tupimwe vilevi kabla hatujaingia humu ndani. Unaweza kujenga hoja yako bila kutukana, huhitaji kutukana ili waziri atekeleze madai yako,” alisema mbunge huyo.

Tags

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hivi wewe Esta bulaya kweli ukamfananishe Magembe na tishu, fikiri kabla ya kutenda esta, usiropoke ropoke tu hata kama ni upinzani sio kutamkatamka tu ilimradi useme, wewe mwenmyewe hushikiki wewe halafu ukamfananishe mwenzako na tishu na wewe tukufananishe na nini tujuze huna akili kabisa wewe

    ReplyDelete
  2. jamani wabnge matusi gani ya rejareja hayo kuweni wastaarabu esta jike zima ovyoooooo nfyuuuuuuuu ufuzi du

    ReplyDelete
  3. Bungeni hakuna umri kila mbunge ni sawa
    CCM acheni ujinga
    Heshima ya umri ipo nje ya bunge
    Na kuitana, mdogo wangu,nwanangu.
    Mwanafunzi wangu ni maneno ya kipumbavu bungeni
    Tunataka hoja na siyo longa longa
    Ukitaka uitwe prof nenda chuo kikuu
    Bungeni wote niwabunge bila kujali umri
    Mbona rais anatumbuwa watu kuzidi umri wake hamsemi
    Fyuuuuu
    Bahati yenu magufuli
    Lakini yupo chama kibovu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hongera Ester
      Jumanne kwani Nani uzee jimboni kwake na ccm bungeni kazi tu

      Delete
    2. Mdau..majipu yako. Yanadhihirisha upeo WA akili yako na malezi uliyopata...POLE TENA SANA!!!

      Delete
    3. yaani wewe mdau wa 11.27am ni mpumbavu sana tena sana usiyejitambua hizo lugha za bungeni unaona ziko sawa? jitambue ndugu yangu usiwe lofa na limbukeni

      Delete
  4. Abdallah Ulega!! Nakubaliana na wewe.. Heshima ni kitu cha bure! Wote mliokuwa hapo ni Waheshimiwa.. Basi kama ulivyo wakumbusha wenzetu.. Nidhamu lugha ya maneno na upangiliaji wake pia ni vitu muhimu na inaimarisha uhusiano bora wa mtu na mtu. na hapo mlipo..Nidhamu na mahudhurio ya mwili na akili ni kitu muhimu na heshima baina yenu ni muhimu zaidi.. Hoja haziletwi kwa lugha chafu zaidi ya kujionesha utovu wa nidhamu na ukosefu wa maadili.. kama nilivyo una na kushangazwa na kikao cha pili munge anabishana na kuto fata amri ya mwenyekiti wa bunge na akawachwa ndani ya bunge... Hii kweli ni sawa!! na bado wanaendelea bila kujifunza au kuhisi kwa hivi sivyo tunavyo tegemewa na wananchi.. Wazo lako ni ZURI na inabidi Getini waangaliwe na akiwa mbunge intoxicated siku anakatwa na posho hakuna.. TUNATAKA BUNGE LENYE WATU SALAMA NA WENYE MWANKO WA MAENDELEO BILA KUJALI ITIKADI ZAO KIVYAMA... nAKUPONGEZA KWA rai yako nzuri na fikra njema Abdallah...

    ReplyDelete
  5. Abdallah Ulega!! Nakubaliana na wewe.. Heshima ni kitu cha bure! Wote mliokuwa hapo ni Waheshimiwa.. Basi kama ulivyo wakumbusha Wenzako( Waheshimiwa).. Nidhamu/ lugha / Maneno na upangiliaji wake] Hivi vyote ni vitu muhimu na kikawaida inaimarisha uhusiano bora wa mtu na mtu ( na hapo mlipo..Nidhamu na mahudhurio ya mwili na akili ni kitu muhimu na heshima baina yenu ni muhimu zaidi.. Hoja haziletwi kwa lugha chafu zaidi ya kujionesha utovu wako wa nidhamu na ukosefu wa maadili.. kama nilivyo ona na kushangazwa na kikao cha pili mbunge anabishana na kuto fata amri ya mwenyekiti wa bunge na akawachwa ndani ya bunge... Hii kweli ni sawa!! na bado wanaendelea bila kujifunza au kuhisi kwa hivi sivyo tunavyo tegemewa na wananchi.. Wazo lako ni ZURI na inabidi kamati ya nidhamu na usalama bungeni ije na mikakati ya usalama ikiwepo uhakikishaji kuwa hawaingii na silaha za moto au baridi hapo Getini waangaliwe na akiwa mbunge intoxicated siku anakatwa na posho hakuna... TUNATAKA BUNGE LENYE WATU SALAMA NA WENYE MWANKO WA MAENDELEO BILA KUJALI ITIKADI ZAO KIVYAMA... NAKUPONGEZA KWA rai yako nzuri na fikra njema Abdallah...

    ReplyDelete
  6. Hongeraaaaaaaaaaaaaaaaaaa Bulaya,,,, hilo sio tusi, kama wanataka matusi wamuone Nape na Lusinde............
    Hongera sanaaaaaaaaaaaaaaa bulaya jike dume usiogopa walafi wa nchi hii

    ReplyDelete
    Replies
    1. huyo bulaya ni jike dume au ni jike la halima mdee??????

      Delete
    2. Hiiiii Baby

      Delete
    3. Anasaga mama yako?
      Au mkeo au wewe
      Fyuuuuuuu

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad