Feza na Lulu Wajitosa Kwenye Bifu ya Vanessa na Shilole

Msanii wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Feza Kessy wamejitosa kwenye bifu la Shilole na Vanessa Mdee ambalo linaendelea katika mitandao ya kijamii.

Chanzo cha bifu ya Shilole na Vanessa hakijatambulika, lakini wawili hao toka jana wamekuwa wakirushiana maneno makali na vitisho katika mitandao ya kijamii hali ambayo imewafanya baadhi ya wasanii kuingilia kati sakata hilo la aina yake.

Muigizaji mahiri Elizabeth Michael ‘Lulu’ alikuwa moja kati ya msanii wa kwanza kutupia neno kwenye ugomvi huo kwa namna ya kushangazwa na jinsi watu wanavyosifia uzuri wao kupitia mitandao ya kijamii.

“Hebu nikazane kusoma nianze ligi za kikubwa na dada zangu wenye madegree na ma masters kama ‘Esilovey’ hizi ligi nyingine zinasikitisha,” aliandika Lulu kupitia Twetter huku akiongeza post nyingine kwa kuandika “Watu wanashindania uzuri, makalio, followers, nguo, outings, umaarufu, umaarufu wenyewe kama network ya mtandao unaokuwaga mpya, full kukatakata,”

Pia msanii wa muziki na mtangazaji wa Choice Fm, Feza Kezzy baada ya kuona stori inakuwa kubwa katika mitandao ya kijamii, aliandika ya moyoni kuhusu jinsi watu wanavyo shabikia mambo yasiyo na maana na kuacha kushabikia mambo ya msingi.

“Yaani watu wa ajabu sana, inabidi mbadilike. Watu wakifanya mazuri or kazi nzuri hamsemi, hamsupport, lakini umbea comments karibu laki moja dah. It’s very sad, bongo we need to change and support our talents Not tear them apart, Ntawacheka sana mkigundua labda hata ma star hawa hawana beef lol,” aliandika Feza kupitia instagram.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Beef ni Beef tu hata kwenye Nchi kubwa kabisa Duniani kama Marekani kuna ma beef itakuwa Bongo???? Acheni hizo, binadamu ni wale wale hakuna cha kusikitisha wala nini. Kama mtu kaleta za kuleta ni lazima watu wanao follow yeye wa support, hii maneno ya kusema eti Wabongo mnasikitisha ni uzushi mtupu kwa sababu huku majuu tunayaona mengi kuhusiana na hayo mabifu, ya Wabongo ni cha mtoto.

    ReplyDelete
  2. Huyo aliyeandika umaarufu wa kukatakata ye mwenyewe shombo kunuka...unawasema wenzie wanashindania nn na ww unafanya nn...kwan we na husna maulid mlikuwa mnashandania nn usijione yo so perfect while in real sense yo just a bastard like others. ..si ndo tasnia yenu mlivyo ama??

    ReplyDelete
  3. wewe feza kwa kuwa na wewe ni mbongo, anza kubadilika wewe, usiseme wabongo kwni wewe sio mbongo!!

    ReplyDelete
  4. lulu mnafiki tu si afadhali hao wana beef zao za kidada kuliko wewe usiye na utu wala adabu kuweka beef na mama kanumba! toa kwanza boriti jichoni kwako! mbwa mkubwa!

    ReplyDelete
  5. Hello what is going on between shishi baby and v money like seriously,you guys look like sisters and it's not good for you to fight kila mtu anahishi maisha yake na business zake sasa chKufia nini jamani daah maybe your guys share love or not.

    ReplyDelete
  6. Hello what is going on between shishi baby and v money like seriously,you guys look like sisters and it's not good for you to fight kila mtu anahishi maisha yake na business zake sasa chKufia nini jamani daah maybe your guys share love or not.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad