Waziri Mkuu Mstaafu,Fredrick Sumaye ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Mwenyekiti wa Chadema – Taifa Freeman Mbowe,amekiambia Kikao cha Kamati Kuu jana kuwa, anampendekeza Sumaye kuwa mjumbe wa CC kwa lengo la kuimarisha chama hicho.
Amesema, dhamira ya Chadema ni kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi ujao, kwa kutumia kila mwanachama kufanya kazi ya uenezi.
Kamati Kuu imeridhia uteuzi wa Sumaye kuwa mjumbe wa Kamati Kuu.
Naye Sumaye amemshukuru Mbowe kwa kumteuwa kushika nafasi hiyo na kuahidi kukitumikia chama hicho kwa nguvu zake zote.
Mhh..Huyu Sumaye fedliki. Mimi nashanga ile wazifa aliipeewa awali ilikuwaje na sasa CDM anaongoza..Duniani kunamambo..haya yetu macho na masikio..
ReplyDeleteWahenga walinena Mfa Maji Haishi kutapa taps..Madalaka Yana majukumu je utayaweza?? Manake lazima uwe na afya. .. Endelea kama unajiamini..nakushauri watolre nje uangalie afya yako Ni bora kulijoni
Delete