Siku chache zilizopita, Gardner alionekana katika kipande cha Video akisherehesha tukio la kumsaka mrimbwende wa chuo cha Tanzania Institute of Accountancy (TIA) jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa “yule binti sina tatizo naye, nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi…”, kisha wimbo wa ‘Ndindindi’ wa Jay Dee ukachezwa na DJ.
Kama ilivyokuwa kwa Lady Jay Dee aliyetoa siku saba za kuombwa radhi kupitia kwa mwanasheria wake Amani Tenga, Gardner amejibu kupitia mwanasheria wake Stephen Axwesso.
Katika barua yake kwa mwanasheria wa Lady Jay Dee, mwanasheria huyo wa Gardner amekiri kuwa ni kweli mteja wake alizungumza maneno hayo alipokuwa katika shughuli iliyotajwa, lakini alidai kuwa hakuna sehemu aliyomtaja mkewe huyo wa zamani.
Alisema kuwa madai ya upande wa Lady Jay Dee hayana mashiko na alimshauri mwanasheria huyo kupitia upya sheria inayozungumzia wanandoa waliotalakiana ili aweze kumshauri vizuri mteja wake kuhusu suala hilo.
Nakala ya barua hiyo pia imetumwa Clouds Media Group na kwa Rais wa Wanafunzi wa Chuo cha TIA.
Na ile sentensi yake isemayo"SINA UGOMVI NA JIDE"NIMEMKOJOZA MAIKA 15"Sasa najuiliza siipati picha ya huyo wakili wa Gadner aliposema kuwa "HAKUNA SEHEMU ALIYO MTAJA MKEWE HUYO WA ZAMANI"Sasa amtaje mara ngapi mara mbili nn?Mawakili wa bongo hao tamaa ya pesa tu wakati yeye mwenyewe anaona mteja wake amepotea step lakini kwa kuwa ana tamaa ya pesa bado anampa matumaini kuwa ni no sweat hakuna kosa alilofanya
ReplyDeletesafiii Gadna, usijirahisishe yeye alivyokutukana kwenye nyimbo yake hakukutaja jina,
ReplyDeletealivyokwambia wewe kichaa aliona rahaa. kajibiwa ukweli kakimbilia kwa mwanasheria.
ReplyDeleteNdindindiiii
ReplyDeleteMnajidhalilidha tu.
ReplyDeleteHapo ni ngoma draw.......Jide ktk NDINDINDI kaimba 'chizi huwa haponi' hakumtaja mtu jina, wadau tunajua anamzungumzia nani, sasa huyo 'chizi' nayeye hakumtaja jina mtu, shida iko wapi??...au ukweli unauma?
ReplyDeletebado wanatafuta kiki
ReplyDelete