Giggy Money: Gardner Kwangu Hachomoki

MUUZA nyago kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Giggy Money’ amefunguka kuwa mtangazaji maarufu Bongo anayeuza maneno katika Kituo cha Redio cha Clouds FM, Gardner G. Habash hachomoki kwake na hadi sasa wako kwenye uhusiano wa mapenzi kwa muda wa miezi sita, Risasi Jumamosi  linakumwagia ubuyu wote.

Akichonga na gazeti hili baada ya picha zinazomuonesha akiwa kwenye mapozi ya kimahaba na Gardner kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Giggy alisema mtangazaji huyo amekuwa mtu wa muhimu kwake kwa sasa.

“Kwani kuna tatizo nikiwa na Gardner? Yule ni mtu muelewa na sahihi kwangu, ninafikiri kupitia yeye nitajifunza mambo mengi na kuzidi kufanikiwa kwa sababu yeye ni moja kati ya watu ambao wako kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu,” alisema Giggy Money.

Gazeti hili lilimtafuta pia Gardner ili aweze kufungukia ubuyu huo, alipopatikana alisema;
“Nipo karibu na Giggy lakini hatuna uhusiano wa kimapenzi, kwa hiyo kama anasema hivyo si kweli lakini yeye ni shabiki wangu na mimi ni mshabiki wake, ninapenda pia kazi anazozifanya,” alisema Gardner.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ka feli maisha Gadner kama kweli anatembea na Gigy,,huyo ni sawa na mwanae Carine ambaye yupo chuoni kwa sasa tafuta age yako maisha ya songe,,,kiki za kibwege hazina maana kwa sasa,,,we dont care if u fuck her but think twice,,,

    ReplyDelete
  2. Udaku muacheni huyo mwanampotevu kidogo apumue maana mmemkalia kooni pumzi hapati kila siku magazetini ni yeye damn!!!! Give her a break for God's sake

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad