Gigy Money: Niko Kwenye Uhusiano wa Kimapenzi na Gardner Kwa Miezi 6 Sasa

Gigy Money na Mtangazaji Gadner G Habashi

MUUZA sura kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Giggy Money’ amefunguka kuwa mtangazaji maarufu Bongo wa Clouds FM, Gardner G. Habash hachomoki kwake na hadi sasa wako kwenye uhusiano wa mapenzi kwa muda wa miezi sita.

Gigy mefunguka haya baada ya picha zinazomuonesha akiwa kwenye mapozi ya kimahaba na Gardner kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Giggy alisema mtangazaji huyo amekuwa mtu wa muhimu kwake kwa sasa.

“Kwani kuna tatizo nikiwa na Gardner? Yule ni mtu muelewa na sahihi kwangu, ninafikiri kupitia yeye nitajifunza mambo mengi na kuzidi kufanikiwa kwa sababu yeye ni moja kati ya watu ambao wako kwenye tasnia ya burudani kwa muda mrefu,” alisema Giggy Money.

Gardner alipotafutwa ili aweze kueleza kuhusu ishu hii alisema:

“Nipo karibu na Giggy lakini hatuna uhusiano wa kimapenzi, kwa hiyo kama anasema hivyo si kweli lakini yeye ni shabiki wangu na mimi ni mshabiki wake, ninapenda pia kazi anazozifanya,”.

Source: Tanzania Today.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya kaka ngoja tuone mwisho...sisi tupooo tu hahahahahaha daaah...

    ReplyDelete
  2. huyo jamaa kachanganyikiwa na pombe, Gigi Money siyo mtu wakuwa naye, na mwanamme akiwa na Gigi Money basi huyo jamaa atakuwa kichaa hajielewi

    ReplyDelete
  3. sasa nimejua wanaume wa kibongo wanapenda tako tu siyo sura tofauti na hapa ulaya ninapoishi hapa wanaume wanapenda sura tu kuliko tako na Gigi maney sura hana, analo tako tu kama wabongo wanavyopenda he he

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kila mtu ana taste yake ya ulaya yaache ulaya ya bongo tuachie wabongo

      Delete
  4. Mkojoleshe nae huyo ukimaliza tafuta mwingine,,,,Ndindiii Mirembe umeshushwa,,,

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad