Hawa ndio Wafanyabiashara Wakubwa wa Sukari Nchini

Rais Magufuli ana vita pevu kuhusu mstakabali wa sukari na hatima ya viwanda vya sukari nchini.

Sukari yote nchini inayoagizwa kutoka nje kwa kiasi kikubwa ilikuwa inaagizwa na hawa matajiri wakubwa nchini kama wanavyoonekana kwenye picha.

Hawa ni baadhi ya matajiri ambao wanamiliki soko la sukari nchini ambalo wakati wa utawala wa Rais Kikwete, hakuweza kuwadhibiti ili kuvilinda viwanda vya sukari nchini na afya za walaji.

Hawa kwenye picha hapo chini ni aina ya watu wanaoitwa sugar industries movers and shakers katika jumuiya ya wafanyabiashara nchini.

Kutoka kushoto ni Harun Daudi Zakaria ambaye juzi vikosi vya usalama nchini vilikuta kwenye magodauni yake huko Mbagala na Tabata tani zaidi ya 4,600 ambazo inasemakana zilikuwa zimefichwa, kwa lugha ya kisheria wanasema hoarding commodities. Huyu wakati mwingine alikuwa anapewa vibali ambavyo waingereza wanasema special/exclusive permit kununua au kuagiza sukari kwa ajili ya soko la Zanzibar.

Anayefuatia ni Said Salim Bakhresa ambaye hununua sukari nchini au kuagiza nje ya nchi maelfu ya tani za sukari kama malighafi kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa kwenye viwanda vyake.

Anayefuatia ni Reginald Mengi ambaye ana viwanda vya vinywaji. Hununua sukari nchini au kuagiza nje ya nchi maelfu ya tani kama malighafi kwa ajili ya viwanda vyake mbali mbali.

Anayefuata ni Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete ambaye baada ya kushindwa vita ya sukari kutokana na nguvu kubwa waliyonayo hawa wafanyabiashara, akaamua kuacha mbuzi ale kulingana na urefu wa kamba yake. Huu ulikuwa ni mwanzo kwa serikali kushindwa kufahamu kiwango cha sukari kilichoko ndani ya nchi na pia kiwango kinachohitajika kwa mwaka.

Anayefuata ni Gulam Dewji ambaye ni Baba yake na Mohammed Dewji (Mo Dewji). Huyu ni Mwenyekiti wa MeTL Group na Mnunuzi na mwagizaji mkuu wa sukari kama malighafi kwa ajili ya viwanda vyake na pia kuuza kwenye soko laTanzania Bara. Huyu pia alikuwa anapewa special/exclusive permit ya kuagiza sukari

Wa mwisho ni Balozi wa Jamhuri ya Djibouti-Tanzania, Saidi Amin Shamo ambaye ni mmoja wa inner circle ya Sir Andy Chande (Mtanzania wa kwanza kukiri kuwa Mwanachama wa Freemasons). Kwenye inner circle ya Sir Andy Chande huwezi kumkosa Edward Lowassa, Rostam Aziz na Balozi Juma Mwapachu.

By Msemakweli
Jamii Forums
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kazi ipo Mwenyezi Mungu mlinde Rais safari ni ndefu na ngumu lakn tutafika salama Amen...lazma tifike kwenye nchi ya ahadi ya maziwa na asali

    ReplyDelete
  2. duu! kazi ipo kweli haya yote ni kwaajili ya kuleana watu wanaona kumnyonga mtu wa hali ya chini ni haki naomba sheria za nchi za kiarabu zihamie tz ili watu wanyongwe hadharani nchi itakaa sawa hata watu wanapotumbuliwa watu hawataki hivi wanataka nini tumekuwa tukinyanyasika muda mrefu tumepata mkombozi bado watu kama kina tundu lisu hawataki ukombozi mwacheni jpm arekebishe nchi

    ReplyDelete
  3. jpjm AMESHAANZA KUWASHUGHULIKIA NA NA iMANI KUWA wAISLAMU WATAUPOKEA MWEZI WA MFUNGO NA SUKAIRI ITAKUWA BWELELE.. jpjm TUOKOE BABA.... HAYA NI MOJA YA YALE MADUDU MADU YALIYOKUWA VIPELE MWANZO

    ReplyDelete
  4. Kila chenye mwanzo lazima Kina mwisho. Sasa ni saa ya ukombozi na tunaamini watanzania tunaamini hivyo na kushikamana pia kuchukia mabaya yote yanayorudisha nchi yetu nyuma

    ReplyDelete
  5. Do maana dingi hakuweza kuiongoza nhi na kujitumbua mwenyewe. Atashikwa kupitia mtoto, mkewe, marafiki na matatajiri wengine. Alikuwa kila sehemu. Sikujua alihusika kwenye sukari pia. Ingawa nilisikia minon'gono ya madini Songea na marafiki wa Africa ya kusini, Uda, Vituo vya mafuta, ESCROW, na Mabasi. Huku kote katajwa na Kupitia Umoja wa wanawake, Ingawa mkewe kisha ropoka. Majengo ya Kigamoni.
    Haya, Tumwachie magufuli na tumuone atatumbuaje donda ndugu hili.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad