Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kaimu Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala David Langa alisema.
‘Kumekuwa na malalamiko mbalimbali kutoka kwa wagonjwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii juu ya huduma zinazotolewa hospitali moja ni lile lililotokea mnamo tarehe 23/03/2016 lililotolewa kwenye gazeti la Mwananchi la Bi Asha Soudy mwenye umri wa miaka 17 aliyejifungulia chooni‘ – David Langa
‘Yule binti alipoambiwa aende kubadilisha nguo maana utararibu wetu kabla ya kutoa huduma zetu kwanza tunamtaka mtu anayepatiwa huduma zetu kwenda sehemu husika, sasa yule binti baada ya kupewa ruhusa alijikuta anajifungulia chooni ndipo taarifa zikaenea kuwa ni uzembe wetu ambapo si kweli’- David Langa
‘Na tukio la tarehe 30/03/2016 lililotolewa na mitandao ya kijamii kuhusu hospitali ya Amana kuhusika na kifo cha Mtoto kilichotokana na kucheleshwa kupata huduma Bi. Mariam Hassan, Malalamiko haya yameshafanyiwa kazi na watumishi waliohusika wameshachuliwa hatua za kinidhamu’ – David Langaa