Idadi ya Ajali zilizojitokeza wakati wa Majaribio Mabasi yaendayo Haraka

Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umesema kutozingatia sheria za barabara za mradi wa mabasi hayo, kwa vyombo vingine vya moto vimesabisha ajali 14 wakati madereva wa mabasi hayo wakiendelea na mazoezi kwa ajili ya kuelekea kipindi cha mpito cha mradi kinachotarajia kuanza hivi karibuni.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala huo, Mhandisi Ronald Rwakatale amesema kuwa ajali hizo zimejitokeza wakati madereva wa mabasi ya mradi wakifanya mazoezi na kisha vyombo vingine vya moto viingilia barabara zake na kusabisha ajiali hizo.

Amesema ajali hizi ni matokea ya vyombo vingine vya usafiri kama magari madogo, daladala, bodaboda na waenda kwa miguu wamekuwa wakiingilia barabara za mabasi hayo na kusabisha ajali kutokana na kwamba barabara hizo haziruhusu mabasi hayo kupisha na vyombo vingine.

Mhandisi Rwakatale amesisitiza kuwa barabara za mabasi hayo ambazo ni za zege zimejengwa mahususi kwa ajili ya mabasi hayo hivyo madereva wa vyombo vingine wanahitajika kuheshimu sheria zinazoongoza mradi huo na kupita katika barabara walizotengewa na watakaokiuka sheria itachukua mkondo wake.

Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka unatarajiwa kuanza kipindi cha mpito mwezi huu wa Mei kutoa huduma ya usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Madereva wapewe semina ya jinsi ya kutumia barabara. Ushamba mzigo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad