Jela Miaka Mitatu Kwa Kumchoma na Pasi Mwanaye

Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela mkazi wa Ukonga Mombasa, Christina Yoram (31) baada ya kupatikana na hatia ya kumjeruhi mtoto wake wa kambo wa kiume wa miaka 11 kwa kumchoma na pasi.

Mshtakiwa huyo pia alimpiga sehemu mbalimbali za mwili mtoto huyo na kumsababishia majeraha.

Akisoma hukumu hiyo jana Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan alisema mahakama hiyo imetoa adhabu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi dhidi yake uliotolewa na mashahidi watano.

“Vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto bado ni tatizo katika jamii, hivyo kutokana na mahakama yangu kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, mshtakiwa utatumikia kifungo cha miaka mitatu jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizi,” alisema Hakimu Hassan.

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, Wakili wa Serikali Chesenci Gavyole aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa wanawake wengine wenye tabia mbaya kama yake. Kabla ya hukumu hiyo, mahakama hiyo ilitoa nafasi kwa mshtakiwa huyo kujitetea ili isimpe adhabu kali.

Katika utetezi wake, aliiomba mahakama hiyo impunguzie adhabu kwa madai kuwa ana Ukimwi, watoto watatu na mama yake mzazi wanaomtegemea na kwamba mume wake amepooza mwili kwa kiharusi.

Awali Wakili Gavyole alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Machi 20, 2013 eneo la Ukonga Mombasa Wilaya ya Ilala.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Laanakhum na huko atakopelekwa hiyo miaka mitatu fresh akabakwe na mademu wenzake ili aone mwenyewe kuwa unyanyasaji ni unyama kudadeki zake malaya mbovu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad