Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Madee amesema wimbo huo ni historia ya kweli ya P Funk na mwanamke ambaye ndiye mama wa mtoto wake wa kwanza, Kajala Masanja.
“Haya yote maisha imetokea kipindi ambacho bado nipo na P Funk, alafu P Funk ana matatizo na mama mtoto wake Kajala, kwa hiyo wakati mi naenda pale kurekodi cheza kidogo, kabla sijamalizana na ile nakutana na beat ya yote maisha inaplay, alafu inaplay na chorus lakini hakuna verse, lakini the way ile beat inavyoplay majani anavyoiimba anaimba kwa feelings kinoma, nikamwambia bwana hii nyimbo mbona kali nigaie niimbe akasema hii na chana mwenyewe babu,” alisema Madee.
Madee aliendelea kusema baada ya mazungumzo P Funk alikubali kumpa beat na kwenda kuifanyia kazi, baada ya kukumbuka Madee mtindo alioutumia kwenye nyimbo zake.
“Sema wewe ulivyochana kwenye kazi yake mola kuna ryhmes fulani naona unapita pita, unaongea kimajonzi hebu chukua hii beat kaandike, kwa hiyo nikapewa ile beat, aliniambia kwamba hii nyimbo ina feeling zangu, nataka uandike kitu hiki na hiki, kwa hiyo idea iliyotoka mule ni idea ya P Funk,” alisema Madee akimuongelea P Funk Majani.