Kibarua cha Rais wa Brazil Chaota Nyasi, Apigiwa Kura ya Kutokuwa na Imani Naye

Kitumbua cha Rais wa Brazil, Bi. Dilma Rousseff kimeingia mchanga.

Baraza la senate limempigia kura ya kutokuwa na imani naye. Hiyo inamaanisha kuwa atakaa benchi na kupelekwa kortini. Bi Rousseff anatuhumiwa kulaghai hesabu za kifedha ili kuficha deni la umma linalokua kabla ya uchaguzi wa mwaka 2014, kitu anachokanusha.

Maseneta walipiga kura 55 za kumuondoa katika mkutano uliodumu kwa zaidi ya saa 20. Ni 22 tu ndiyo waliokuwa upande wake. Makamu wa Rais, Michel Temer atakaimu nafasi yake wakati kesi ya Bi Rousseff ikianza kusikilizwa.

Kesi hiyo inaweza kuchukua siku 180 hiyo inaamanisha kuwa atakuwa amesimamishwa katika kipindi ambacho michuano ya Olimpiki jijini Rio de Janeiro itaanza, August 5.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tanzania tutaweza haya ???????????????????

    ReplyDelete
  2. Tuweze wapiii ndugu katiba inamlinda kiongozi kama malaika...only in tz...

    ReplyDelete
  3. Hiyo ndio demokrasi(democracy)ya ukweli ukikosea hata uwe nani una step down na ikiwezekana unasimamishwa mbele ya hakimu ujibu mashtaka yako na mwishoni ukikutwa na hatia ni jela au faini kubwa kwenye nchi kama yetu bongo jambp hilo ni ndoto za alinacha"UNDUGUNAZATION"too much ndio maana kila aingiaye madarakani anaendelea kufisadi pale alipoachia yule mwenzake aliyemtangulia

    ReplyDelete
  4. all except JON POMBE MAKUFULI/FULL STOP. Who wanna say NYOKO..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad