Kigwangalla Amtaka Gardner Aombe Radhi kwa Kumdhalilisha Lady Jaydee

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangalla, amemtaka mtangazaji wa Clouds FM, Gardner G Habash kumuomba radhi aliyekuwa mke wake, Lady Jaydee kwa ‘kile alichokiita’ kama udhalilishaji kwake na kwa wanawake wote.

Wikiendi iliyoisha imesambaa video mtandaoni ikimuonesha mtangazaji huyo akiongea kwenye tamasha alilokuwa mshereheshaji: "My name is Captain Gardner G Habash all the way from Clouds FM, Jahazi hatari sana. Na sina neno na yule mtoto wa kike. Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi.”

Video hiyo imesababisha hasira kubwa kwa mashabiki wa Jaydee na watu wengi kwa ujumla.

“Ndg. Gardner amefanya udhalilishaji mkubwa si tu Kwa @JideJaydee bali ametukana wanawake wote. Mimi #BaloziWaWanawake namtaka aombe radhi,” ameandika mheshimiwa Kigwangalla kwenye Twitter.

“Natoa rai kwa uongozi wa @cloudsfm kumtaka Ndg. Gardner afute kauli yake na aombe radhi kwa @JideJaydee na kwa umma ili kulinda heshima yao,” ameongeza.

“Jamani, sijui ugomvi wao wala sina interest ya kujua, sema alichokisema G na nikasikia ni katika tusiyosemaga hadharani kwa heshima ya mama,” amefafanua.

“Sina maana wamchukulie hatua. Watambue tu kosa lake na wamtake kwa heshima kwa mama aombe radhi. Mimi ni mtumishi namba 2 kwenye Wizara inayosimamia ‘mambo ya wanawake’! I know what I am talking about hapa.”

Video Hii Hapa

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wakati jdee kamuimba Gadna kuwa ni mwendawazimu haponi na kampeleka milembe hamkuona tusi, ila kajibiwa imekuwa issue.

    ReplyDelete
    Replies
    1. USIKURUPUKE,ALITAJA JINA GADNER NI MWENDAWAZIMU?KUMUIMBA MTU BILA KUMTAJA JINA AU KULINGANISHA MATENDO YAKE SIO TUSI WALA HUWEZI KUMSHTAKI MTU ETI KAKUTUKANA KWA WIMBO PASIPO KUTAJA JINA.G KAHUSISWA MOJA KWA MOJA KWA KUWA WIMBO ULIOPIGWA NI WA JIDE,HALAFU NDIE MKE ALIYEISHI NAE KWA MIAKA 15.

      Delete
  2. Naibu waziri anzia bungeni kwanza kwa kile kijitoto kijibunge cha ccm kilichotukana wabunge wa ukawa wanawake
    nusra video toa tena toa

    ReplyDelete
  3. ccm wasenge sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. CCM IMEINGIAJE HAPO WE MWENDAWAZIMU?

      Delete
    2. Kumbe inauma ccm imeingia kwa sababu ni waziri toka ccm katokeo
      yale ya baby bungeni hakusema
      kasema hili la mtu mmoja
      Magufuli una kazi

      Delete
  4. Acha ujinga utafutwa na kukamatwa au umesahau sheria za na makosa ya mtandao. Kama usenge ni mzuri basi anza wewe uone ulivyo siyo una msakizia ccm. Shwin wewe mtoto wa mtaani una baba wala mama na ndiyo maana unaandika ujinga. Nenda shule itakusaidia kuelewa mambo mengi ila mahali popote ulipo dola itakukamata sasa uone msenge nani wewe, au ccm.

    ReplyDelete
  5. KI UKWELI ANATAKIWA AADHIWE KWA KUWATUSI WANAWAKE WOTEE!!!NAWASHANGAA SANA WANAOMTETEA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad