Kuongea Kiingereza ni Kipaji – Shilole Afunguka

Msanii wa muziki, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kwa kudai kuongea Kiingereza siyo kitu cha mchezo kama watu wanavyofikiria.

Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television Jumatano hii, Shilole alisema yeye amepigana mpaka ameweza kuongea Kiingereza.

“Kiingereza ni kipaji jamani, mimi naongea Kiingereza wakati ambao najisikia. Lakini asikwambie mtu, kuongea Kiingereza ni kipaji,” alisema Shilole.

Muimbaji huyo ameachia kazi mpya iitwayo ‘Say My Name.’
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu ni mnafiki hajui kabisa kuongea kithungu. anawadanganya watu au ndo kiki hizo.

    ReplyDelete
  2. du! umeeanza kujisifia eti unaongea kingereza? ops kwa ile sentes moja alokufundisha Idriss. rudi shule unatia aibu sana.

    ReplyDelete
  3. Umependeza Mwangu!!

    ReplyDelete
  4. Majuto mjukuu walisema waswahili wakati mmepelekwa shuleni na wazazi wenu ili mkasome mliwaona wazazi ni wapuuzi mkawa hamuhudhurii masomo ipasavyo utoro mwingi au kutozingatia masomo na kusahau elimu ni hazina ya maisha yako ya baadae sasa mmeishakuwa wakubwa ndio mnaona kumbe mlifanya ujinga mkubwa ambao haufutiki maishani ng'oo kwa kutohudhuria shule ndiyo hsyo maneno kama eti kuongea kiingereza ni kipaji hahahahaaa!we kiboko kama ungesoma inavyotakiwa wala husingepata tabu ya kuongea kuandika hiyo lugha lakini pia unaweza ukaenda kwenye evening class ukajiendeleza ila uwe na nia na dhamira shule iwe shule sio shule na party utatoka tena sifuri bi mdogo

    ReplyDelete
  5. kingereza ni lugha kama kizaramo tuuuuuuuuuuuuu
    hata Waingereza wengine hawakijui vizuri kama watanzania wasiujuwa kiswahili

    ReplyDelete
  6. shame on you, you better go back to kindergarten my dear you are talking nonesense

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad