Rais John Magufuli amepata heshima ya pekee kualikwa na waziri mkuu wa Uingereza katika mkutano utakaofanyika kuzungumzia mikakati ya mapambano ya rushwa ikiwa ni nchi mbili tu zimepata fursa hiyo kwa bara la Africa ikiwemo pia Nigeria.
Lakini Rais wetu amedai sasahivi amebanwa na majukumu kwahiyo atawakilishwa na Waziri mkuu mh. Kassim Majaliwa
Chanzo: Cloudz Tv
Kwa hili la Kukataa Mwaliko wa Uingereza, Rais Sikuungi Mkono
14
May 10, 2016
Tags
Sawa sawa, waziri wake mkuu anatosha kabisa hata huko wingereza, muwakilishi ni waziri mkuu, Raisi yuko busy na majukumu ya nyumbani kuiletea maendeleo, kwani akianza kutoka toka mafisadi papa ni wengi watapata miyanya, hongera Raisi wetu mpendwa, msadizi wako waziri mkuuu anatosha kabisa kukuwakilisha, chapeni kazi tu, wananchi tuna Imani nanyi, wewe na Waziri wako wote mmbarikiwe kulitoa taifa hili kwenye usingizi mzito
ReplyDeleteZilizoalikwa ni Nchi mbili tu kutoka hapa Bara la Afrika, Nigeria na Tanzania, kwa sababu ni Nchi zinazoongoza kwa Rushwa katika Bara hili yaani Nigeria na Tanzania. Huo ni udhalilishaji wa hali ya juu sana kwa Taifa ambalo Rais wake anajitahidi kupigana usiku na mchana dhidi ya Rushwa. Kwa kweli ni Halali yake yeye Mheshimiwa Rais JPM kuutolea nje huo mwaliko.
ReplyDeleteBy the way Waziri Mkuu wa hapo Uingereza ametoka kuzidhalilisha baadhi ya Nchi zilizoalikwa kwenye huo Mkutano wa Rushwa kwa kumwambia Malkia Elizabeth II kuwa kuna Nchi mbili zinazoongoza kwa rushwa Duniani Nigeria na Afghanistan zinaleta wawakilishi wake. Sasa wako wanamshambulia juu ya hizo comments zake na kumuomba huyo Waziri Mkuu David Cameron aombe msamaha kwa comments zake dhidi ya hizo Nchi mbili yaani Nigeria na Afghanistan. Viongozi wa hizo Nchi mbili wamechukizwa sana na hizo comments na kuziita kuwa ni za udhalilishaji mkubwa sana. Nadhani Mheshimiwa Rais JPM aliishastukia hayo maneno na ndio kwa maana akautolea nje huo mwaliko.
ReplyDeleteBy the way Waziri Mkuu wa hapo Uingereza ametoka kuzidhalilisha baadhi ya Nchi zilizoalikwa kwenye huo Mkutano wa Rushwa kwa kumwambia Malkia Elizabeth II kuwa kuna Nchi mbili zinazoongoza kwa rushwa Duniani Nigeria na Afghanistan zinaleta wawakilishi wake. Sasa wako wanamshambulia juu ya hizo comments zake na kumuomba huyo Waziri Mkuu David Cameron aombe msamaha kwa comments zake dhidi ya hizo Nchi mbili yaani Nigeria na Afghanistan. Viongozi wa hizo Nchi mbili wamechukizwa sana na hizo comments na kuziita kuwa ni za udhalilishaji mkubwa sana. Nadhani Mheshimiwa Rais JPM aliishastukia hayo maneno na ndio kwa maana akautolea nje huo mwaliko.
ReplyDeleteHakuna sababu ya kualikwa ulaya ili uambiwe au ufundishwe namna ya kupambana na rushwa. Muandishi unasema raisi "amepata heshima ya pekee"
ReplyDeleteSasa hiyo heshima ya pekee mbona siioni. Heshima ya pekee rais aliyo ifanya ni kukaa numbani na kuwatumikia wananchi wake.
JB Kalugira
haina tatizo kabisa,watanganyika hamna shkrani kabisa na wengi ni majipu,mwacheni kabisa magufuli afanye yake,mungu akulinde baba na wabaya wote wenye nia mbaya.
ReplyDeleteNyinyi hamuelew nini alicho kuwa anatafut huy mwandish, yaani alimpigia Lowassa kampeni kubwa na kumchafua Magufuli ila akashinda uchaguz sasa jamaa anaona kweli kumb alikua anajidangany sasa walisha mteg rais mitego ming ili wapatt pakuanzia kumudhalilish wanapakosa sasa kalet hiy hoja et kapat heshim ya kipekee,kwan wakat anaapa rais Uingera iliwakilishwa na nani? mbon wazir wao mkuu hakuja? ach na sisi tuwaonesh kam hatushtuki ten na mwaliko zote ni inchi na huru kama huji kwang unawakilishw hamna budi na mimi nitawakilishw poa Pombe. Huy mtoa habar mbin za kumchafua rais wet zimemuishia sasa anatafut tu sababu zisiz na mpango.
ReplyDeleteAlichofanya Muheshimiwa JPM ni sahihi kabisa, si kila mwaliko lazima uhudhurie, maana ya kuwa na wawakilishi ni nini? Mbona hatuoni viongozi wa mataifa makubwa kama USA nk wakihudhuria kila mialiko, Utanzania kwanza, ni viongozi wasio wazalendo ndio wanakimbilia kimbilia nchi za ulaya wakati nyumbani wana matatizo kibao, misiba, ajali, mafuriko, rusha nk. Address challenges za nyumbani kwanza
ReplyDeleteUPUUZI UMEANDIKA,
ReplyDeleteMIMI NILIDHANI KAKATAA KABISA HUO MWALIKO KUMBE KAMPA WAZIRI MKUU AWAKILISHE SASA HAPO KUNA UBAYA GANI?NAMUUNGA MKONO JPJM.
Heshima gani kwani anamlipa nauli? Waziri mkuu kalipa kaenda Waziri mkuu mwenzie. Kwanza mkutano wa kuwekwa kikaangoni na madharau wa nini.
ReplyDeleteWatanzania wenzangu huwezi kusafili na ukaacha famiria yako ina matatizo,pili kumbukeni Mheshimiwa Rais Magufuri kakabidhiwa Nchi ikiwa haina pesa, majipu nayo mengi,wafanyakazi hewa wengi,sukari nayo inafichwa ,akisafiri mafisadi atayapa nafasi,baba mheshimiwa Rais enderea na kazi zako za maendereo na Nchi yetu ;HAPA KAZI TU RAIS HASAFIRI.,Beaty Semuguruka
ReplyDeleteNina uhakika rais angekuwa mtu wa kwenda safari za nje sana wewe ndio ungekuwa wa kwanza kuhesabu safari zake.UMEROGWA WEWE.
ReplyDeleteUNADHANI AKIACHA YEYE KWENDA AU KUWAKILISHWA NA WAZIRI MKUU HIZO SAFARI AU MIALIKO TUTAKOSA NINI WATANZANIA?TAFUTENI TU KILA NENO LA KUMPAKAZIA JPJM ILI TUMCHUKIE,ILA WENYE MAPENZI MEMA NA TZ HATUSIKILIZI HUO UPUUZI WENU,TUNAMPENDA MAGUFULI,TUNAMUOMBEA KWENYE NYUMBA ZA IBADA NA HATA MAJUMBANI KWETU.MUNGU MBARIKI JPJM NA VIONGOZI WOTE WENYE MAPENZI MEMA NA MAGUFULI.
ReplyDeleteUMETUMWA?
ReplyDelete