GODBLESS Lema, Mbunge wa Arusha (Chadema) leo amemwaga sumu bungeni kuhusu staili ya utawala wa Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi.
Amesema, kwa namna Rais Magufuli anavyoendesha nchi, taifa linahitaji maombi ya haraka kuhakikisha anarudishwa kwenye mstari wa maadili kwa manufaa ya nchi.
Akisoma Makadirio na Mapato katika Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Lema ambaye ni msemaji wa kambi ya upinzani kwenye wizara hiyo amesema, Rais Magufuli ataumiza watu wengi.
“Wakati Taifa letu linapita kwenye changamoto nyingi kama vile ukosefu wa sukari, umeme, umasikini, mizigo kupungua bandarini, madini ya Tanzanite kuanguka bei na ubadhirifu uliokithiri katika mfumo wa utawala. Rais mwenyewe ameonekana kufuatilia na kufanyia kazi habari za kwenye mitandao ya kijamii.
“Kwa tabia hii ya Rais Magufuli, kama Taifa tunahitaji maombi haraka, kwani Rais ataumiza watu wengi sana kwa kufuatilia maneno ya mitaani kwa njia mbalimbali , kwani kwa madaraka aliyonayo Rais bila shaka ataumiza watu wengi.
“Mfano, Sakata la Mke wa Waziri Mahiga na Trafiki barabarani. Ni jambo dogo sana na la karaha kuona linazingatiwa na Rais,” amesema Lema.
Amesema, haikuwa busara Rais Magufuli kukemea familia ya waziri wake mbele ya vyombo vya habari na kuagiza askari huyu kupandishwa cheo bila kujua historia ya utumishi wake.
Lema alikumbusha kwamba, wabunge walipoanza vikao vya Kamati za Bunge, vyombo vya habari vilimnukuu Rais Magufuli akielezea mpango wake wa kuanza kurekodi mawaziri wake wanaolalamika juu ya staili yake ya uongozi.
“Kwa hiyo leo ukienda kwenye ofisi za mawaziri unaona, hofu, mashaka, kutokujiamini, mambo yatakayo punguza ufanisi, ubunifu na uhuru katika utendaji wao, jambo linalopeleka Taifa kuzorota katika nyanja zote kwa utumishi wa umma jambo ambalo ni hatari kwa Taifa,” amesema.
Akizungumzia mashaka ya nchi Lema amesema,
Taifa letu liko katika mashaka na kuwa, serikali inaufahamu ukweli huu.
“Taifa hili lina utulivu unaosabishwa na hofu inayojengwa kwa mabavu na silaha na sio amani, kuna mateso makubwa wanayoyapata wananchi wa Taifa hili kila siku, umasikini, njaa, ukandamizwaji, ubaguzi, uonevu, udhalilishwaji na mateso ya jinsi mbali mbali kutokana na kukosa uongozi unaojali maisha ya Watu,” amsema na kuongeza;
“Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni baada ya uchambuzi na tathimini ya “Hali ya Usalama na Amani ya Nchi yetu” kabla wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015, tumebaini kuwa nadharia na mwenendo wa demokrasia ya vyama vingi hapa nchini iliwekwa kando.
“… na badala yake sura nzima ya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015, uligeuka kuwa ‘Military Operation’ yaani ‘Operesheni ya Kijeshi’ kwa kisingizio cha kulinda amani.”
Lema amesema, mnyonge anayelia moyoni kwa huzuni ya kuonewa ni hatari kwa usalama wa nchi na dunia na kwamba, vikundi vingi vya uhalifu duniani kwa asilimia kubwa vimesababishwa na utawala wa kibabe, uonevu na ukandamizwaji usiovumilika na huko ndiko tunakoelekea kama Taifa.
Amesema, “matendo mabaya haya yaliofanyika wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita Zanzibar na Tanzania Bara ni ishara ya watawala kuelekeza Nchi yetu katika mapigano ya sisi kwa sisi katika siku za usoni.
“Unapokuwa na Jamii inayoamini kuwa mfumo wa demokrasia hauwezi kuwapa wananchi viongozi wanaowataka, maana yake ni dhahiri kwamba unaanza kuifundisha jamii hiyo kufikiri njia mbadala ya mabadiliko katika Nchi.”
Amesema kuwa, Tume ya Uchaguzi inayotiliwa shaka na jamii ni hatari kwa usalama wa nchi na kwamba, ni muhimu kwa taifa kutafakari uwepo wa katiba ya wananchi na Tume Huru ya Uchaguzi itakayorudisha imani ya Wananchi katika uchaguzi wa kidemokrasia.
“Mungu adhihakiwi apandacho mtu ndicho avunacho, utulivu mnaouona Zanzibar na kwingine kokote kule kuliko na ukandamizaji ni nafsi zinazojadili mwelekeo mpya wa maisha yao katika utawala wa nchi yao.
“Zanzibar mmeshinda uchaguzi kwa hila na sio kwa haki, wekeni kumbukumbu maneno ya Kambi Rasmi ya Upinzani leo kuwa, ipo siku Zanzibar itakuwa ni sehemu ngumu ya kuishi binadamu kama hamtachukua hatua sasa ya kurekebisha mlichokifanya Zanzibar na Tanzania Bara katika uchaguzi uliopita,” amesema.
Hata hivyo amehoji kwamba, kwa namna mambo yanavyoendeshwa nchini, je kuna matarajio ya taifa kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020 kwa njia ya kidemokrasia?
Chanzo:Mwanahalisi
Lema Amwaga Sumu Bungeni Kuhusu Staili ya Utawala wa Rais Magufuli..Adai Taifa Linahitaji Maombi
7
May 17, 2016
Tags
KAZA BUTI JPM HAO KINA LEMA WANATAKIWA WAKACHUNGUZWE AKILI KAMA ZIKO SAWASAWA AMA KUNA KONEKSHENI AMBAYO IMEPONYOKA AKILINI MWAKE LEMA TENA TAMBUA KWAMBA SERIKALI ILIPOFIKIA INAHITAJI RAIS KAMA MAGUFULI VINGINEVYO NCHI HAIWEZI KUENDESHWA KIHOLELA KAMA ILIVYOKUWA HUKO NYUMA KWAMBA MWENYE NACHO NDIO KILA KITU SERIKALINI UMEFIKA WAKATI WA MABADILIKO NA MTU ANAYEWEZA KULETA MABADILIKO YA KWELI HAPA NI MAGUFULI PEKE YAKE WENGINE WATASUBIRI SANA LEMA TENA FYATA HUO MDOMO WAKO NGUVU YA WANACHI NI KUBWA ZAIDI KULIKO HUO MDOMO UNAFIKIRI UKISEMA HIVYO ATATETEREKA HATETEREKI TUNAZIDI KUMPEND NA TUTAMPENDA NASISI WANANCHI WA HALI YA CHINI TUKONYUMA YAKE NA TUTAMLINDA KWA KILA HALI POLE SANA LEMA UMEPOTEZA KALOLIZI ZAKO NYINGI KWA KUONGEA VITU AMBAVYO HAVIMSHAWISHI MTU HAPA KAZI TUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUMPAKA KIELEWEKE KAZA BUTI BABA PAMOJA SANAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA MABADILIKO KWA MAGUFUI TUNAYAONA
ReplyDeleteGodless lema, Jina lako ni Zuri. Nimeisoma Rai yako... Una Uhuru wa kuichambua unavyo ona sawa kiupeo wako.. Lakini mimi sikubaliani nawe katika mengi ya uliyo zungumza.. Imedhihirisha kuwa Neno Demokrasia maana yake hujaielewa ipasavyo ( Niko tayari kukuelimisha ukihitaji) Fikra Potofu umeonesha katika maoni yako ( Kudhihirisha kuwa wewe ni kambi ya upinzani) umejaribu kuweka mada ya Zanzibar iweze kuboost hoja na kupata ushabiki ( Hilo ni lako kisiasa ) Ndugu Mheshimiwa ikiwa huu wewe umeona kuwa itatia wasiwasi uchaguzi wa 2020 ni kwamba huna imani ya kizalendo kwa Taifa letu ( hapo ningekuomba urudi nyuma hatua kumi na kuanza kuangalia watu wali karibu na wewe katika kata yako / kijiji chako na mji wako na uwasikilize maoni yao na Kasi yetu na Nia yetu uliwemo wewe oia mfaidikaji wa mwanzo katika kulihudumia taifa letu hili na wananchi wake.. Uchaguzi wa 2020 uko mbali uombe mungu akupe umuri uuone na uamuzi wake ni wananchi mimi na wewe / huyu na yule / hawa na wale.. Na tumuombee mungu ampe afya JPJM Utamchagua kwa nini... NI MCHAPA KAZI MUAMUNIFU MUADILIFU NA MZALENDO MWENYE NIA NJEMA YA KUTUTUMIKIA... KIBOKO YAO WATU WANAOJIJUA KUWA...(UNAWEZA KUMALIZIA) WEWE NI MWANASIASA UNAYE HITAJI KUJIFUNZA NA KUIJUA SIASA.. KWA TAARIFA YAKO SIASA NYINGIIIII FAIDA YAKE HATUJAIONA.. WEWE SERA MIMI SERA MWISHO TUANZISHE UBISHI HALAFU ,..... NI UVIVU TUU .HATUYATAKI HAYA JITUME . WAJIBIKA .KUWA MKWELI NA MZALENDO.. PALIPO HARIBIKA UNATENGEZEZA SIO UNAKOSOA NA KUANGALIA FULANI AJE ATENGENEZE... JPJM TUMEMPA JUKUMU LAKINI NI WAJIBU WETU SISI SOTE KUMSAIDIA KATIKA UTENDAJI ILI AWEZE KUTUFANYIA MAZURI ZAIDI NA SIYO KUMCHOSHA KWA KILA DOGO NA KUBWA .. WE NEED TO BE POSITIVE AND RESPONSIBLE CITIZENS.
ReplyDeleteFaki Sosi / Mwanahalisi...We need More Professionalism when reporting and Choosing the Right Heading.. Cause our Waheshimiwa like to see such Heading but when you go throgh! is just another cabbage in the bin. Hakuna kichwa wala Miguu.. Upoteshaji mtupu background knowledge is jero 00000
ReplyDeleteJamani huyu si ndio yule Lema wa Alusha? Na yeye pia mwanasasa Chipikizi!!
ReplyDeleteSehemu kubwa ya maelezo haya hapo juu ni upuuzi mtupu. Yameandikwa na layperson we expect much more from opposition. Swala la police brutality, rampant corruption in all police departments, Dar police traffic wanakusanya pesa Tu. Dear UKAwA MPs anzeni kutumia akili zenu Lowasa is dying politician msipotezi muda wenu kwake.
ReplyDeleteMimi siku zote nimekuwa nikisema upinzani unakwisha kabisa nchini mwetu, hivi ni kweli Lema hajui taratibu na kanuni za bunge? je nin nini kinachomsukuma kufanya hivyo wakati wanasema wanae katibu mahili aliyekuwa kinara wa migomo ya madaktari, lakini pia bungeni yupu kiongozi wa kambi ya pinzani Mhe,Mbowe, ina maana hutuba hiyo haikupitiwa kabla? jamani opposition mmechoka na uenda mnaendea kubaya. Chama tawala kimegundua tatizo lenu kubwa ni kutojua taratibu na kanuni na ndiyo maana wameweza kuwabana na si kutumia nguvu. Mnawezaje kuongoza nchi wakati sheria na kanuni tena za bunge zinawapiga chenga? Dr Maghufuli yupo sahihi kwa taifa kama letu lilipokuwa limefikia kitu ambacho wao pia wanalifahamu vizuri ila tatizo ni kutaka waonekane wanafanyakazi na kujijenga kisiasa nasema katika hali ya kawaida huu si ustaarabu, na ujue duniani kote hakuna nchi inajititoshereza kwa asilimia 100. Lema aache siasa namtaka asome historia ya USSR kwa sasa Russia na hasa viongozi wanne, ambao ni VI Lenin,Joseph Stallin,Vladimil Putin na Msaliti Michael Ghobhaechev. Ukiwasoma hawa wote kwa makini utaona Upinzani mnavaa viatu vya kiongozi gani niliowataja na Dr Maghufuli analinganishwa na kiongozi gani niliowatajia. Acheni siasa ambazo zinakosa mpango mkakati kwani mnapotea na kuanza kuchekesha na kufanya vituko kila kukicha. Siasa ni sayansi siyo uana-harakati.
ReplyDeleteLema kamwaga ushuzi sio sumu tumechoka na siasa za matukio wamekosa dira wapinzani kwani Magu anayafanyia kazi yale enzi ya Kikwete kukicha ndio ilikuwa wimbo wao kuwa serikani haina memo sasa muziki umebadilika na wao wanabadilika na kuwatetea mafisadi na majizi kweli tutafika tunakokwenda au tutegemee bla bla za wanafiki
ReplyDelete