Lulu Michael Awapa Makavu Mastaa Wapenda Kiki

STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa mastaa wengi wanapenda kiki kuliko kusaka fedha kitu ambacho yeye hakifanyi.

Akizungumza na gazeti hili, pasipo kuwataja majina, Lulu alisema anashangazwa na tabia ya mastaa wengi kuwa ‘bize’ kutafuta kiki kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii badala ya kukutana pamoja na kufikiria ni kitu gani wanaweza kufanya ili waendelee kimaisha.

“Jamani mimi nashangaa siku hizi huku mjini mastaa wanatafuta kiki sana kuliko kufikiria mbinu ya kusaka hela yaani ni shida kabisa, tubadilike jamani, muda unakwenda,” alisema Lulu.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwenda huko wewe mwenyewe ndio wa kwanza kutafuta kiki kwenye mitandao. Sasa unaona wenzako wanakuja juu na watakufunika sasa ndio unaanza kujishau. Kwanza ni nani aliyekuambia kuwa Pesa ndio kila kitu katika maisha. Acha ujinga nenda shule ukafute ujinga na pia uache wivu wa kijinga dhidi ya wenzako. Hata hivyo muda wako wa ku shyn umekwisha waachie wengine wafanye vitu vyao......Domo kubwaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  2. Jini mauti naeee

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad