Lulu Michael:Mastaa Bongo Mtaishia Kuchambana Instagram tuu

ZA uso laivu! Staa mwenye mvuto Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa mastaa wengi Bongo wataishia kuchambana kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram badala ya kutafuta elimu ili siku moja wapate nyadhifa serikalini.

lulu2342 (1)

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Lulu alisema kwamba, amegundua kuwa elimu ndiyo kila kitu hivyo amewasihi mastaa wenzake waache kuchambana na kutuma picha kwenye mitandao ya kijamii badala yake watafute njia ya kujikwamua kielimu.

“Jamani mmemuona mwanamama mwenzetu Dk. Tulia alivyojinyakulia unaibu spika? Hiyo ndiyo raha ya elimu. Mastaa kazi kutukanana kwenye mitandao ya kijamii na kuweka picha, mwisho wenu utakuwa hivyohivyo,” alisema Lulu.


Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. KAMA UMELIONA HILO CHANGAMKA NA WEWE!!!

    ReplyDelete
  2. Nitakuona mjanja kama ukimaliza hiyo shule na kupata vyeti then uanze kufanya hiyo kazi and not only bla bla shule bla bla action is the best than talks

    ReplyDelete
  3. Mwenzenu kauza akili
    Wala si sura wala umbile

    ReplyDelete
  4. wewe mwenyewe Lulu mbona ndiyo namba one kuweka picha mitandaoni kila kukicha halafu unawasema wenzako

    ReplyDelete
  5. Jini mauti shut up....

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad