"Ninafanya kwa niaba yenu, ninafanya kwa niaba yenu, ningekuwa sifanyi kwa niaba yenu, na mimi ningeingia madarakani ningeanza kushirikiana na hao, na wengine walifikiria nitashirikiana nao, wamekwama mimi nitawatumbua kila siku ili Tanzania iwe ya neema iweze kwenda mbele, haiwezekani nchi kama hii tajiri, Tanzanite ipo, dhahabu ipo, wanyama mpaka nyani wameanza kuuzwa, wakimalizika nyani si tutauzwa na sisi ndugu zangu, ni lazima nisimamie hili" amesisitiza Dkt. Magufuli.
Aidha katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amewahakikishia kuwa serikali yake imeanza kuwashughulikia wafanyabiashara ambao wameficha sukari kwa makusudi na kusababisha upungufu wa bidhaa hiyo.
Rais Magufuli amesema tayari vyombo vya dola vimekamata tani 5,000 za sukari iliyofichwa na mfanyabiashara mmoja huko Tabata Jijini Dar es salaam na pia vimembaini mfanyabiashara mwingine aliyeficha sukari hiyo Jijini Arusha.
"Kweli nitawakomesha hawa, wasije wakanilaumu, haiwezekani ukaficha sukari wakati viwanda vyetu vinatengeneza sukari, kuna mmoja mwingine yupo Arusha hapa, nae ameficha sukari, alienda akanunua kwenye viwanda vya sukari vya hapa akaificha yote, leo ninamshughulikia.
"Kuna mwingine alinunua sukari pale Kilombero zaidi ya tani 3,000 akaficha, na mwingine ameshikwa pale Tabata alikuwa ameficha tani 5,000, na wanasubiri katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili ndugu zetu Waislamu wapate shida, haya ni mashetani makubwa, unawafichia watu chakula ambacho wanatakiwa kula, lakini nataka niwahakikishie ndugu zangu, hili ni tatizo la muda Tanzania, sukari itapatikana kwa wingi, na itanunuliwa na serikali, tumeshaagiza sukari lakini hatutawapa vibali hawa wafanyabiashara ambao wanatunyonya, tutanunua wenyewe na tutauza bei ya chini, hilo ndio lengo la serikali" Amesema Rais Magufuli
Blessed Sir!!!...
ReplyDeletesafi sana mheshimiwa sisi tunakuunga mmono na miguu yote ndani ya kumina nane futa vibali vyao wote watakaobainika kufucha sukari serikali ya awamu iliyopita ilikuwa hivyo kabisa walitazama matumbo yako na ya watoto wako sasa kila lililo na mwanzo lina mwisho wake asante mungu kwa kutuletea mtetezi wetu wanyonge utatawala mika mia moja
ReplyDeleteAgree wit you.. Lakini Mia Itakuwa tumemchosha Sana. ..yeye itabidi tupeleke nuswada jweny Bunge kumpa kipindi cha nyongeZa cha najeruhi miaka 5 kwa mnatakwa ya wananchi..ssema Hilo Bunge lenyewe hata siwaamini hivvyo. Manake wako kwenye baby 👶 laivu not laivu..na posho zetu za kodi wanakula kiulaini. Inaniuma hii Na kunisikitisha.. Manake wanatuchelewesha safari yetu ya mbali..hawajui Hilo Na Kama wanajua basi wana nia ambato itabidi kuitafakari uoya au vp mdau...hapa kazi tu
Delete