Mahakama ya Kisutu Yatoa Hati ya Kukamatwa kwa Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar imetoa hati ya kukamatwa kwa Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob (Pichani)kutokana na kutofika mahakamani.

Meya huyo anakabiliwa na shitaka la kumshambulia  mwandishi wa Habari wa gazeti la Uhuru, Christopher Lissa na kumsababishia maumivu makali.

Kesi hiyo jana ililetwa mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwa ajili ya usikilizwaji ambapo upande wa mashitaka ulikuwa na shahidi mmoja.

Wakili wa serikali Onolina Mushi alidai kwamba,kesi hiyo ililetwa kusikilizwa lakini mshitakiwa pamoja na wakili wake hawajafika mahakamani.

Kutokana na hali hiyo,aliiomba mahakama itoe hati ya kukamatwa kwa mshitakiwa huyo pamoja na kupanga tarehe nyingine ya kuendelea kusikiliza shauri hilo.

Hakimu alikubali maombi hayo ikiwemo ya kutolewa hati ya kukamatwa kwa Meya huyo.Kesi hiyo iliahirishwa hadi Mei 23 mwaka huu kwa ajili ya usikilizwaji.

Katika kesi hiyo,Boniface anadaiwa kutenda kosa hilo  Septemba 11, mwaka jana, maeneo ya Kinondoni, Dar es Salaam, kipindi hicho akiwa na cheo cha Udiwani kata ya Ubungo.
Ilidaiwa kwamba,mshitakiwa huyo alimpiga Lissa kwa mateke na ngumi sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha makali.

Shitaka la pili ilidaiwa kwamba ,mshitakiwa huyo katika tarehe hiyo kwa makusudi na kinyume cha sheria aliharibu kamera aina ya Nicon yenye thamani ya sh. milioni nane mali ya Kampuni ya Uhuru Publication Limited.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ma ccm yanayomuamgusha magufuli yanaanza sinema mbofu mbofu

    ReplyDelete
  2. hayatafika mbali!

    ReplyDelete
    Replies
    1. pumbavu zenu kama mtu amefanya makosa kwa nini asiwajibishe, na sheria zipo mambo ya ccm yanaingiliaje na sheria kuchukuwa mkondo wake acheni ushabiki wa kipumbavu fuatilieni issue kabla hamchasema ujinga wenu.

      Delete
  3. Wasira alitukana, mkapa pia hata Kikwete Ccm hata haikusema chchote.Ccm ni ileile, mfumo ni uleule, wafanyskazi hewa ni ufisadi wao,majipu mamuu ya nchi bado huru na yako serikalini. Magufuli bado anatumbua dagaa changa, mibabu ya usisadi yajishafisha kijanja mali zao zafichwa, na wabunge wengi wamekaa bungeni ni mizigo elimu finyu na uhuru na demokrasi inakufa tunamwenda kiudecta wa mtu mmoja. Ndugu raisi tunakumba tendea hami nchi na mamilioni ya watanzania leta katiba ya wananchi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hiyo ndio tabu yenu nyinyi 'machoko wa ukawa', mnawaona hao 'mbwa wenu' kama malaika vile, wasiguswe hata kama wamefanya makosa....Wasira na Mkapa walipotukana nani damu ya nani ilimwagika? Huyo 'mdudu' wenu alipiga magumi na mateke,tena walimchangia ofisi yote ya chadema, wakataka kumwua lakini Mnyika akasema tukimuua watatushtukia kwa vile walimwona akiingia ofisini.......leo hii unasema 'fyoko-fyoko', kama huna ulijualo funga bakuli lako....mfyuuuu

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad