JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata wasichana 15 katika nyumba iliyopo maeneo ya Ukonga, waliokuwa tayari kusafirishwa kwenda Oman kufanya kazi za ndani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi wa kanda hiyo, Simon Sirro, alisema wasichana hao walikamatwa baada ya Polisi kupata taarifa toka kwa msiri kuwa kuna mtu amewaweka wasichana kwa ajili ya kuwasafirisha.
Sirro alisema Polisi walifuatilia na kufika katika eneo hilo na kufanikiwa kuwakuta katika nyumba ya Hadija Mohamed (40) wakiwa wamegawanywa katika vyumba viwili.
Alisema uchunguzi wa awali, umebaini kuwa mwanamke huyo anashirikiana na mwenzake Salma Habibu (43) mkazi wa Temeke kuwatafutia masoko nchini Oman na wao ni mawakala wanaoletewa kutoka mikoani na kuwapokea kwa ajili ya kuwasafirisha.
Aidha alisema watuhumiwa hao watapelekwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
Pia ametoa onyo kwa watu wenye tabia hiyo kuacha, kwani wasichana hao wakifikishwa nje ya nchi hufanyiwa vitendo vya kikatili na unyanyasaji.
Katika tukio jingine, Polisi kanda hiyo imewakamata vijana 75, ikiwa ni muendelezo wa msako wa vijana wanaofanya matukio ya wizi wa majimbani nyakati za usiku.
HAO WANAWAKE WAPEWE HADHABU KALI!!!
ReplyDeleteUlizeni uganda na Kenya. .wasichana masikini wanauwawa bila kosa. .mama mmoja wa kiganda rafiki yangu,mtoto wa dada yake kauwawa last week.na maiti ikasafirishwa uganda..wala hawaisindikizi .jamani tuwatahadharisheni wasichana kupelekwa hasa Dubai wanarudishwa maiti.
ReplyDeleteni kweli wengi wao wanateswa tunayasikia na wengi wao wanakwenda na ushirikina sasa pale wanapokamtwa ndio ina kuwa shida ingekuwa vizuri kufungua ofisi za ma agent na wanapo kwenda omani au kwengineo ikiwa anapata mateso ina kuwa ofisi zina shughulika. ushirikina wao ndio unaowaponza na hii ya ushirikina nimesena kwa sababu nineona ama ya kutesa kiumbe hata mimi napinga ila naomba musiwavunjie riziki
ReplyDeleteacheni kuongea kitu msicho kuwa na uhakika nacho, hakuna anae teswa ila kwa sababu flani(umalaya,kunyanyasa watoto wa maboss wao, kutembea na waume za watu)msiangalie upande mmoja tu kwani hata huko tanzania watu wengi wa nje wananyanyaswa sana.Wahindi na warabu wengi wanao wekeza katika nchi ya tanzania wanafanyiwa matukio mengi sana na wananchi kama vile kuwaibia mali zao au kuwachomea mashamba na manyumba yao.
ReplyDeleteAcheni kutoa habari za uongo Oman inawafanya karibu million mbili toka nchi mbali
ReplyDeletembali hakuna aliyekimbia kwa kuteswa au kuuliwa