Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema kauli ya Rais John Pombe magufuli ya kuzuia kuingizwa kwa sukari kiholela nchini ilikuwa ni katika kulinda viwanda vya ndani.
Aidha Majaliwa amesema kuingia kwa sukari Tani 70,000 toka nje ya nchi hakutaathiri uzalishaji wa viwanda unaotarajiwa kuanza mapema mwezi julai.
Akijibu swali la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na mbunge wa jimbo la Hai, Freeman Mbowe, Majaliwa amesema uhaba wa sukari ni tani 100,000 na uwezo wa viwanda kuzalisha ni tani 320,000 huku mahitaji ya sukari kwa mwaka mzima ni tani 420,000.
Amesema katika kukabiliana na uhaba uliopo Serikali kupitia bodi ya sukari imeagiza sukari nje ya nchi na tayari Serikali imeshaanza kupanga mikakati ya kudumu ya kumaliza tatizo la sukari kwa miaka ijayo.
Akiuliza swali la nyongeza Mbowe alimtaka waziri mkuu kuwahakikishia watanzania kuhusu bei elekezi na kutaka kujua ni lini uraismu wa uanzishwaji wa shamba/kiwanda eneo la bagamoyo utakavyo malizwa.
Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema swala la kuanzisha shamba katika eneo la bagamoyo lina mchakato mrefu na halina urasimu wowote.
Amesema shamba hilo limepakana na mbuga ya saadani na kwamba linategemea sana maji ya mto Wami, lakini pia wanyama nao wanategemea maji ya mto huo.
Hivyo amesema serikali na wadau wanaendelea kuangalia suala hilo kwa umakini ili kutoa maamuzi yatakayo leta tija kwa taifa.
Kuhusu bei elekezi ya sukari amesema tayari bodi ya sukari imeshaanza kusimamiasuala hilo, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale wote watakaopandisha sukari kiholela
Majaliwa: Rais Magufuli hakukosea kuzuia sukari kuingia nchini kiholela2
2
May 19, 2016
Tags
Kila siku watu sukari sukari, kwanza mshukuru hayo madhara ya sukari ni mengi. Kuriko maitaji hiyo misukari ya kutoka huko nje wameijaza mitoxin (mikemiko) mpka na hapo hapo utakuta hao wafanyabiashara wanachukua ile ambayo muda wake unaotaka kuishiria na kuwaletea huku. Si wanajua huku udhibiti wa vitu kama hivyo ni ziro kama si mdogo, na huku ikifika ni kuweka tu kwenye vinywaji pasipo kuangalia madhara, huku kwetu Afrika si dampo, kwani tunajithamini na elimu ndogo tuliinayo, tumekazana na hiyo misukali ya huko nje, mfanyabiashara yeye hana mpango na madhara anawaza kupata utajili wake tu. Na utakuta kwa kuwa anajua wala haitumii yeye hiyo sukali, yeye atatafuta ya hapa hapa kwetu si anajua ndio iko kiafya zaidi, kwanza organic, haijaisha muda wake kwa matumizi ya binadamu wala haina mikemiko mingi (toxin) tufunguke watanzania blood sugar 2 ni tatizo duniani
ReplyDeleteTutafika, Tutafika Tutafika, Ndg Watanzania tumeanza safari 2016 tuwape hawa ndg waliojitolea kama sadaka watuvushe mto nile then mto jordani kumbuka safari hii ina figisu figisu nyingi kwa hiyo kuna watu wengi watakata tamaa lakini hakika tutavuka jipeni moyo watanzania. Mimi ni mpinzani wa kweli lakini katika safari hii ikiongozwa na haruni lazima niambatane nao.....twendeni don't spare yourself mr opposition lets walk together.
ReplyDelete