Majibu ya Snura baada ya Chura wake Kupigwa Nyundo na Serikali

Baada ya wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo kuufungia wimbo wa Snura, Chura jana, muimbaji huyo anaonesha kutoshtushwa na hatua hiyo hasa kutokana na support anaiyopata kutoka kwa mashabiki wake.

Kwa ufupi haoneshi stress, walau kwa kile alichokiandika kwenye Instagram. “Ingekua ndio hela leo ningekua bilionea lo!!! Nawapenda sana kwakweli na nawatakia usiku mwema,” aliandika Snura kwenye Instagram.

Aliongeza hashtag: #utaipenda2_ndimuimekolea_malimao_kama__210_habarizetuwanazo_ilazaohatuna.”

Pamoja na wimbo huo kufungiwa kuchezwa kwenye redio na TV, Snura aliagizwa kuhakikisha amefuta video zake zote mtandaoni.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lazima aseme hivyo kwani yeye anahasara gani? Yeye hakucheza humo, kawadhalilisha wanawake wenzie kwa 'vijisent vyake', na wao kwa UJINGA na UPUMBAVU wao wakakubali kujidhalilisha......hovyoooooooo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad