Makonda: Wanawake Ndiyo Chanzo Cha Ufisadi Nchini

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wanawake wamekuwa ni chanzo cha ufisadi nchini kutokana na kupokea zawadi zitokanazo na fedha za kifisadi.

Makonda aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnyamani Vingunguti Dar es Salaam jana katika mkutano wa kujadili namna ya kupata mikopo mbalimbali kutoka Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB).

” Ninyi wakina mama mmekuwa chanzo cha ufisadi kwa vile mmekuwa mkipokea fedha na zawadi mbalimbali kutoka kwa watoto wenu lakini mmekuwa hamuwahoji wanako zitoa fedha hizo kwani zingine zinakuwa za kifisadi” aliseama Makonda.

Makonda aliwaambia wanawake hao kuwa hata katika suala zima la usafi linaanzia na malezi ya usafi ya wakina mama kwa watoto wao tangu wakiwa wadogo jambo ambalo lingesaidia kipindi hiki ambapo kunachangamoto kubwa ya kusafisha miji yetu.

Katika hatua nyingine Makonda alitoa pongezi kwa Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto kwa kuwa jirani na wananchi wa kata yake kwa kufanya maendeleo bila ya kujali itikadi za vyama hasa katika kujipatia mikopo kutoka katika Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB).

“Nimefurahishwa na diwani wenu Kumbilamoto kwa kushirikiana nanyi ili  kujiletea maendeleo ni jambo zuri na wakati huu ni wa kukutana kubuni na kuangalia jambo gani litawakwamua kiuchumi badala ya kuwaza maandamano yasiyo na tija” alisema Makonda.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya kina mama tulianzwa kutukanwa bugeni leo mkuu wa mkoa anatutukana wanawake wote wa Tanzania kwani mtu anamlazimisha mwanaume kuhonga si nyege zao zinawatuma
    CCM hiyo jamani fyuuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad