Makontena 115 Ya Sukari Yanaswa Jijini Dar es Salaam....RC Makonda Aviagiza Vyombo vya Dola Vifanye Uchunguzi wa Kina

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kuchunguzwa kwa sukari kontena 115 ambayo ni zaidi ya tani 3,000 iliyokutwa katika bandari kavu ya PMM iliyopo eneo la Vingunguti.

Makonda alitoa agizo hilo jana wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika bandari hiyo na kubaini uwepo wa sukari hiyo ambayo ni mali ya Mohamed Enterprises, ambayo kwa taarifa zake aliambiwa zilikuwa kontena 165.

Alisema anazitaka mamlaka zinazohusika kama Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), pamoja na Shirika la Viwango (TBS) kuichunguza sukari hiyo kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza katika uwepo wa sukari hiyo kama sukari kuagizwa kutoka Dubai lakini imetoka Brazil na imepakiwa Dubai, na upangwaji wa kontena hizo katika bandari hiyo.

“Nashindwa kuelewa kwa nini sukari iagizwe kutoka Dubai lakini itoke Brazil na kufungashwa Dubai inaonesha inaweza kuwa imeshawahi kuisha muda wake hivyo nataka ichunguzwe na tunataka tujue kama Mohamed Enterprises anaficha sukari ili ipelekwe kwa wananchi kwa matumizi,” alisema Makonda.

Mbali na kutoa maagizo hayo, Makonda pia amezuia kutumika kwa sukari mifuko 22,000 iliyokutwa katika ghala la Mohamed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) lililopo Barabara ya Nyerere na kutaka wapeleke vielelezo kuhusu sukari hiyo kwa mamlaka zinazohusika kama ya matumizi yoyote.

Alisema sukari hiyo inayodaiwa kuwa ni ya viwandani ni lazima iangaliwe kama kweli ipo kwa ajili ya mahitaji ya viwandani au ilikuwa itumike tofauti na ilivyokusudiwa.

Kwa upande wake, Meneja Operesheni wa bandari kutoka MeTL, Firoz Ebrahim alisema sukari hiyo imefuata taratibu zote na imefika katika bandari hiyo wiki moja iliyopita.

Katika hatua nyingine, Kampuni ya Al Naeem iliyopewa agizo la saa 36 kuanzia juzi iwe imeshaanza kusambaza sukari kwa bei elekezi iliyokuwa katika bandari ya Dar es Salaam, imeanza kutekeleza agizo hilo jana jioni.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wafanyabiashara wataikimbia na wawekezaji hawatakuja nchini mambo ni magumu sn nguvu inayotumiwa na viongozi ni km ule wakati wa firauni jmn fateni sheria na sio kutaka sifa tu kwa wanachi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwahiyo wewe mdau hapo juu upo radhi kulishwa kulishwa vyakula ambavyo muda wake wa kutumika umeshaisha(expired)kitambo na kufungwa tena upya na kubandikwa tarehe/mwezi/mwaka fake ili vionekane kuwa bado vipo salama wakati sio kweli Je?unayajua madhara ya kula vyakula ambavyo muda wake wa kutumika umeishapitwa na wakati au halafu wewe huyo huyo uje kusema umerogwa baada ya kuugua magonjwa ya ajabu ajabu yaliyosababishwa na hivyo vyakula wakati wa kumlaumu ni wewe mwenyewe kwa kula vyakula vibovu shenzi type halafu dizaini yenu wenye vichwa vya kuku(chicken head)mpo wengi sana bongo shule iliwapiga chenga kitambo

      Delete
  2. DAH KUMBE NCHI HII INA SUKARI YA KUTOSHA!!!!

    ReplyDelete
  3. Wewe anonymous 8:44 ujui ulisemalo wakati wa fulani kulikuwa na wafanyi biashara gani? Hana kinachofanyika ni kuzui wafanya biashara wadanganyifu na ndio kazi ya uongozi kama wewe ulikuwa unataka kuja kuwekeza au kufanya biashara ya udanganyifu basi usije bongo, HAPA KAZI TUU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad