Mama Salama Amtetea Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

SALMA Kikwete, Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete ameonesha kukerwa na wale wanaoshambulia utawala wa mumewe (Rais Kikwete) na kwamba, hakuna sababu ya kufanya hivyo.

Mama Salma alisema hayo jana kwenye mkutano wa Umoja wa Wanawake (UWT) unaofanyika mjini Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa CCM Makao Makuu.

Alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja baada ya kujitokeza hadharani kumkingia kifua mtoto wake Ridhiwani Kikwete kuhusu kuhusika kwake na mkataba wenye utata wa Kampuni ya Lugumi.

“Kila mwaka naendelea kuisemea serikali iliyopo madarakani mambo mazuri, acheni hali ya kukaa na kuanza kusema kwamba serikali ile ilikuwa vile na serikali hii iko hivi.

“Wala msisema yule alikuwa vile na huyu yuko hivi, kwa kumalizia hayo napenda kusema mume wangu ambaye ni mwenyekiti wa CCM Taifa anawasalimia sana,” alisema Mama Salma.

Akizungumzia utumbuaji wa majipu alisema, serikali kwa sasa imeanza kutumbua majipu makubwa kuanzia juu lakini zipo taarifa kuwa, yapo majipu mengine ngazi za chini pia ndani ya CCM.

Alisema, “kila anayejitambua kuwa ni jipu kabla hajafikiwa ni bora akajitumbua mwenyewe au ajipake spriti ili jipu hilo lipoke mapema kabla halijatumbuliwa.”

Hata hivyo alionesha wasiwasi kuwa, kuna uwezekano miradi mingi ya UWT ikachukuliwa kutokana na umoja huo kuwa na mali ambazo zinaonekana kumilikiwa bila kufuata taratibu.

Alisema, kwa upande wa ardhi kuna viwanja vingi ambavyo havina hati na vimekaa muda mrefu bila kuendelezwa jambo ambalo kwa sasa mameya wanaweza kuvibadilishia matumizi.
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. umesha maliza ufesti lady jitulize

    ReplyDelete
  2. Lisemwalo lipo na kama halipo laja.Unaona wazi Magufuli anatumbua yale unayoyatetea ambayo yalitengenezwa chini ya uongoxo wa mumu wako.ama sivyo utumbuaji haungekuwa na haja.laxima yaliuotokea na kutendeka chini ya himaya ya mumewako so yasemwe tu, yatumbuliwe hasa.acha serikali na bunge lofuatoloe kisheria. Unaeadema watu wa chini dingi wao bado kutumbuliwa. Ndiye aliyesababisha haya yote.wachin wimwiga dingi baada ya kuona si mwaminifu na mhusoka pia. Wijua hawatatimbilowa kwani viongozi wengi wa juu wasongefiriki kujitumbua wenyewe

    ReplyDelete
  3. Mama najua kwamba unampenda mume wako lakini ngoja nikukumbushe usemi wa mme wako. " Najua kua bandarini kuna ukiukaji katika utendaji wao" Hakuchukua atu zozote!! !! Watu wengi mnatumia vyeti vya bandia" Hakuna alicho kifanya!! " Wahuza madawa ya kulevya nina wajua!!" Hakuna alicho kifanya!! " Dawa yenu ipo jikoni ina chemka " Pole mama kwa kumtetea mme wako.

    ReplyDelete
  4. Mwanagu Salma... Hii ngoma Nagwa nakusihii kaa pembeni .. Manake cheche zinaweza kuruka kama jiwe la gizani.. Huu ni ushauri wangu.. Tunakupendeni wote ..

    ReplyDelete
  5. Waseme wote hata wewe Salma

    ReplyDelete
  6. Mama Salma Kikwete na mumewe walikua wako busy na safari.Nchi ilikua inajiendesha kwa kudra za mungu

    ReplyDelete
  7. Huyo Mama kwa kweli ana boooreeee sana. Leo hiii mambo yamechachuka ndio anaanza kuzileta story zake. Kwani hakujua kuwa haya mambo yangekuja kujulikana ama kama ni mambo yalikuwa yanawaumiza Watanzania walio wengi na hasa wale masikini. Ni kitu gani alichokifanya kama First Lady kuhakikisha anasimamia matatizo ya watu maskini. Mbona katika maelezo yake hatoi uwiano wa yale yanayozungumzwa dhidi ya yale yaliyotendeka kipindi cha utawala wa Mme wake???? Huyu Mama ni bora akae pembeni ajipumzikie tu, wameishaiharibu hiyo Nchi vya kutosha.

    ReplyDelete
  8. Na ndoo maana nchi za wenzetu ukitaka Urais wanaangalia
    sifa za Mke au Mume

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad