Wimbo huo sasa hautakiwi kuchezwa tena kwenye redio na TV (sina uhakika kama video yake imewahi kuchezwa na TV yoyote). Kwa mujibu wa maelezo kwa vyombo vya habari, Snura ana nafasi ya kuirekebisha video hiyo kitu ambacho nadhani hakiwezekani kwakuwa wimbo nao umepigwa marufuku.
Serikali pia imesitisha ‘maonesho ya hadhara’ ya Snura hadi pale atakapojisajili BASATA.
“Serikali inawataka wasanii kujiuliza mara mbili kabla ya kubuni kazi zao za sanaa. Wafikirie wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wanazipokeaje? Wavae nafasi ya wale wanaowadhalilisha. Waelewe kwamba sanaa si uwanja wa kudhalilisha watu hata kidogo,” yamesema maelezo ya wizara hiyo.
Kwa maelezo hayo inaonesha kuwa Snura ana nafasi ya wazi ya kurekebisha mambo na kuendelea na kazi kama kawaida japo hatoweza tena kuutumbuza wimbo huo uliotrend si tu Tanzania bali nje ya nchi.
Haya ni mambo ambayo nimejifunza kutokana na uamuzi huu na naamini ni somo kwa wasanii pia.
Youtube si kichaka cha kurundika ‘video chafu’
Snura alijua kuwa Chura ni wimbo wa kuweka mbali na watoto na lazima video yake ingezigusa sharubu za serikali kupitia taasisi zake husika kama vile BASATA, TCRA na zingine. Ndiyo maana alisema video yake ataitoa Youtube peke yake, kama alivyofanya Nay wa Mitego kwenye video yake ya ‘Shika Adabu Yako.’ Ni kwasababu imani ya wasanii wengi ni kuwa mkono wa serikali hauwezi kukufikia iwapo mambo yako utayamalizia mtandaoni tu.
Ni kweli kuwa Chura imtrend sana mtandaoni kutokana na clips za video za wanawake wenye mizigo mikubwa wakiucheza kwa madaha. Hakuna anayeweza kubisha kuwa clips hizo pamoja na video yake rasmi imekaa kushoto kimaadili hivyo si jambo la kushangaza serikali kucharuka – ni kitu tulichokitarajia.
Lakini cha muhimu ambacho wasanii wanatakiwa kujifunza ni kuwa si salama tena kufanya kitu controversial ukitegemea kuwa utakiweka Youtube na hakuna atakayejali. Tupo katika nyakati za hatari zaidi sasa hasa kutokana na kupitishwa kwa sheria ya makosa ya mtandaoni ambayo pornography ni kitu chenye adhabu kali huko.
“Serikali inawakumbusha wananchi wote kutojiingiza katika makosa ya sheria ya mtandao kwa kusambaza wimbo huu kwa njia yoyote ile ya kimtandao,” imeonya taarifa ya wizara hiyo. Japo sheria hii haijawa kali sana kwa sasa, bado wasanii wanaweza kupoteza mengi kama wakiamua kufanya vitu vinavyokiuka maadili kwa matarajio kuwa Youtube, Instagram au WhatsApp ni kimbilio na hakuna anayejali.
BASATA haina meno tena?
Awali tulikuwa tumezoea uamuzi wowote wa kufungiwa wimbo au msanii unafanywa na baraza la sanaa la taifa, BASATA au TCRA kwenye matukio machache. Lakini sasa uamuzi huo umechukuliwa na wizara yenyewe, kitu ambacho kimesababisha maswali mengi kuwa iweje uamuzi wa kuufungia wimbo wa Snura umechukuliwa na mamlaka ya juu zaidi! Pengine kuna mabadiliko ambayo sasa yanaifanya wizara kuingia front yenyewe! Hata hivyo kwenye mkutano na maofisa wa BASATA walikuwepo kama watu walioitwa kusikiliza tu.
Video chafu zinaharibu brand
Well, wanasema sex sells, hilo haliwezi kupingwa na ndio maana video nyingi za muziki zenye wasichana warembo wenye vichupi zina views nyingi Youtube. Lakini mara nyingi msanii anapojikuta kwenye mikasa ya kufungiwa kazi zake kwa kigezo cha ‘maadili’ hasa kwa kazi zinazofanana na Chura ya Snura humharibia sifa msanii na brand yake. Matokeo yake katika jamii msanii huyo huanza kuchukuliwa kama ‘aliyeshindikana’ au ‘mhuni’ na kama ikitokea mara nyingi, kibiashara hasa zile kubwa na zinazohusisha makampuni humwathi
Chanzo:Bongo5
Kwa hili sikubalian na wewe mtoa habar ao hiyo wizar, kwa kwel sion kit kichaf kweny video ni kawaid mke ao msichan kutingish mauno, na kam kutingish mauno ni dhambi kwa nini waliumbw kuwa na mauno? kwanz tujiuliz kwel wizara husik huwa inaheshim ao kufuatilia mamb yasio na tija? kwa nini kwa upand wawa sanii wizar huwa inakimbilia sana na kuchukua uamuz harak? kwa nini hay maamuz hatuyaon kweny mamb muhim? shulen watot wanapachikw mimb na waalim wao, ni wat wangap weny pesa zao ao umaaruf ambao wana harib watoto wa shule? mbon pak weny wamefungw myak nend rud wako gerezan mpak hivi hawaj fikishw mbel ya hakim, wizara ngap ambaz zin tuhum fulan ila hatuon maamuz ao hatuwa zinaz chukuliwa? maov ni meng ambayo yana tendwa na waat ambao wangepaswa kuyaheshim il wao ndo mustar wambel kukiuk hak ila hatuon hatuwa zinaz chukuliwa. Kun mamb muhim ya kushurulikia ila hawayaon alaf wanakimbilia mamb yasio na athar zozote. Et amevunj maadili kweli? kwa wat walio som na munakubalian na hil? huwa na wasapoti kweny mamb fulan ila kwa hili hamujamtendea Snura haki. Kam nihivo bas, rushwa, elimu duni ao vyuo vibov, matusi na uonevu, mlo mmoja ao maish mabay. Serekali ichukue hatua kwa haya yote ili mwanadam awe ajisikie kam serekal na wizar zake zinafuat maadili. Akhsanteni.
ReplyDeleteHebu taja jinsia yako kwanza ndio tuendeleeeeeee
DeleteKuna vitu vingi vya kufanya kwenye hili taifa sidhani kama chura ana madhara kwa mtu lakn kwasababu ni chura atavaliwa njuga na yale ya muhimu yataachwa yapite hii ndo tz bwana...sijui nihamishe familia yangu twende duniani kwa wanaojielewa maana hapa tulipo si duniani tupo kichakani...uhuru wa kufanya chochote ilimradi usivunje sheria kwenye hii nchi hakuna tena
ReplyDeleteHebu taja jinsia yako na umri wako kwanza
DeletePamoja na hayo yote ya Snura kuna hao wanaotembea kama hawana nguo wak wanajiona wameva nguo serikali na wizara yake ya kufuatilia maadli munawachukulia hatua gani?
ReplyDeleteMtu akijistiri awapo kazini mnamtafutia sababu ya kimfukuza akivaa nusu uchi ndio heshima
Hapo Chura ana ubaya gani?
Ndio jamii tulivyo
Ya kufundishana mazuri hamyasemi mpka mrushwe roho ma mioyo ndio mnajua kama kuna kibaya.
Kaeni barabarani muone wanawake wanavyovaa au hamuwaoni?
Tafuta mwanamke wa kuoa usitegemee kumalizia shida zako kwa wacheza uchi videoni. Hivi hujiulize kwanini yeye mwenyewe Snura hakucheza kwenye huo wimbo??
DeleteMimi nashangaa sana hii Serikali yetu mambo ya kijinga jinga yanayapa kipao mbele na mambo ya maana wanayanyamazia khaa!
ReplyDeleteHivyo hii video inakosa gani haswa? mmbona kwenye Youtube ni wengi tu wanakatika mauno! kuanzia watoto wa shule na kina Masomange na wengine kibao mbona zile clip zao hazifungiwi au hawaonywi.. hapa kuna uonevu.
Nimesema na nitarudia kusema serikali mambo ya maaana wanayafumbia macho''funika kombe mwanaharamu apite'' hivyo kuna Jumba lilianguka limejegwa chini ya kiwango na wahindi fulani na ikauwa raia wa kawaida (masikini) lakini sijasikia serikali wale wahandisi na matajiri kuchukuliwa hatua yoyote ''wakatuziba ziba siku za kwanza na magazeti yao ya uhuru na Mzalendo mahakama kisha hakuna alie uliza tena! lakini la Sanura na Shilole utasikia mpaka kwenye bunge.
Watanzania mtafanywa mandondocha na serikali hii hadi mkome muanze kujadili wasanii na kina dada poa kisha mkiwasahau mafisadi wa Escaw na TPA ( Bandarini) na n.k
Wewe ni wa jinsia na umri gani?
DeleteWatu wanafurahi kufungwa hiyo video ya chura hawajui iko siku hata hiyo you tube itakuja kufungwa maana kuna vyura wengi ndani ya you tube.Sasa mtu kama hauipendi kwanini unaitafuta kwenye you tube?Mie binafsi siipendi lakini kufungia ni uonevu
ReplyDeleteEti 'siipendi' mnafiki mkubwa, usingeitetea kama huipendi. Walochezeshwa uchi kama wangekuwa ni mama, dada au ndugu yako yoyote ungejisikiaje? Mbona hujiulizi kwanini Snura mwenyewe hakucheza kwenye huo wimbo.......mfyuuuuu
Delete