Mambo ya Msingi Kuyafanya Kabla ya Kuoa/Kuolewa

Ndoa nyingi zinaingia kwenye migogoro kwa sababu ya mambo ya kukurupuka na kufanya haraka bila wahusika kufahamiana vizuri, hebu tuzingatie yafuatayo ili tusiseme 'NINGEJUA NISINGEOA/NISINGEOLEWA'

1. Chanzo cha uhusiano wenu kiwe ni upendo wa dhati
2. Chunguza kwa mwenzio juu ya tabia:nidhamu, adabu, hasira, ulevi na umalaya
3. Mpeane muda wa kutosha kufahamiana
4. Mtembee pamoja maeneo tofautitofauti kama michezoni, bar na out mbalimbali ili muone interest za kila mmoja
5. Muwe wa imani moja. ila kama mmeshibana sana na mwaweza kuvumiliana hata wa imani tofauti ni sawa.
6. Wajue ndugu wa mwenzio ili kupata habari zao zitakazokufahamisha mwenzao pia yukoje
7. Pimeni afya zenu bila aibu. kuna maradhi mengi kama HIV/AIDS na mengine.
8. Kama ni Mkristo au Muislam funga ndoa Kanisani au Msikitini na siyo Bomani.
9.Kwa Wakristo ndoa haina talaka. huu ni mpango wa Mungu. kuachana na kuoa mwingine ni dhambi.

N.B: kama mwenzio ana tabia usiyoipenda, usifunge ndoa naye ukitegemea atabadilika.abadilike wakati mkiwa wachumba na siyo kwenye ndoa, labda kama umeshamkubali kama alivyo
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dah aiseeee!! Ni kweli kabisaaaaaa. Wengne tuliwahi kukurupuka na kuyakuta tuliyoyakuta we acha tu. Sasa umezungumzia kuwa kwa Mkristo ndoa haina talaka "Kwa Wakristo ndoa haina talaka. huu ni mpango wa Mungu. kuachana na kuoa mwingine ni dhambi." Sasa kwa mtu kama mimi niliyewahi kumuoa Muislam lakini tulifunga naye ndoa bomani ndio inakuwaje???? Kwa maana tuliisha talikiana mahakamani. Ushauri Ndugu zangu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad