Marais Duniani Wavutiwa na Vita ya Ufisadi Tanzania

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema viongozi wakuu wa nchi na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Rushwa, wamevutiwa na jitihada ambazo Tanzania imezichukua kukabiliana na janga hilo.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wake kwenye mkutano wa siku moja wa wakuu wa nchi, ulioitishwakujadili suala la kupambana na rushwa duniani uliofanyika Lancaster House, jijini London, Uingereza.

Waziri Mkuu alisema katika kikao cha kwanza, kilichohudhuriwa na wakuu wa nchi na viongozi wa kitaifa wapatao 20, alipata fursa ya kuelezea jinsi Tanzania ilivyoweza kupambana na rushwa kwa kuzingatia vigezo vikuu vinne.

Waziri Mkuu alivitaja vigezo hivyo kuwa ni kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria zinazohusu masuala ya rushwa; uanzishwaji wa mahakama maalum ya mafisadi ambayo inatarajiwa kuanza kazi Julai, mwaka huu; mikakati ya udhibiti wa fedha za miradi ya wananchi na utaratibu wa kubaini wala rushwa kwa kushirikisha jamii ikiwemo kutunza siri za watoa taarifa.

“Ziko sheria ambazo zinafanyiwa kazi hivi sasa ambazo ni lazima zipitishwe na Baraza la Mawaziri kabla mahakama hii haijaanzishwa, zikishapitishwa na Baraza ndipo zitaanza kutumika,” alisema.

Akifafanua kuhusu mikakati ya udhibiti wa fedha za miradi ya maendeleo, Waziri Mkuu alisema kwamba katika bajeti ya mwaka huu, Serikali imeongeza kiasi cha fedha zilizotengwa kwa shughuli za maendeleo kutoka asilimia 27 hadi kufikia asilimia 40.

Waziri Mkuu alisema alipata fursa ya kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron ambaye mbali na kupongeza juhudi za Serikali ya Rais John Magufuli katika kupambana na rushwa, pia aliahidi kutoa mwaliko ili Tanzania iweze kushiriki kwenye mkutano mwingine wa masuala ya rushwa utakaofanyika Japan, Julai mwaka huu.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tunamshukuru Mungu kwa kukupeleka Salama na kukurudisha Salama. Kassim Majaliwa, Sisi Watanzania Tunaimani na kazi yako... Umeweza kutudhihirishia kwamba wewe na Mkuu wetu mko na mwelekeo Mmoja.. ambao si mwingine ila ni wa kutufanyia kazi sisi wananchi kwa masilahi yetu na Taifa letu Nia yenu na lengo lenu ni kutuondoshea adha ndogo ndogo ambazo zilikuwa zinatuandama kila siku si katika Ajira/ Mahospitalini / katika usafiri na hata katika kudhulumiwa ambako ni kinyume na sheria. zikitumika njia mbali mbali zikiwemo / Mikataba hewa/ wafanyakazi hewa / Mashirika hewa / Mishahara hewa na mbinu za kubuni kufanikiwa wizi na ubadhirifu... matokeo yake imekuwa kila mtu asiye yajua au kufanya hayo huwa analalamika lakini sauti yake haiendi mbali.. Lakini awamu hii ya TANO mmeamua kuyavalia njuga.. Na matokeo tunaanza kuyaona si hapa nchini tu, Bali Barani kwetu Africa na Mataifa mengine Ulimwenguni.. Na hii ni Dalili ya kukubalika kwenu na Mataifa ya Ulaya ni wamekubali kwamba Tanzania Wameamua na wanafanya kweli. Rushwa na Ubadhirifu watauondoa na spidi waliyochukua ni inaridhisha na mwelekeo ni kutukwamua sisi Wananchi.. Na umeweza kuwathibitishia kwamba hakuna kulala au kusimama katika hii Safari na next Phase ni kwamba Anti Sabotage Tribunal itaundwa ili tuweze kuwashughulikia Wahujumu.. Hongera kwa hizi hatua na tunawaombeeni Mungu wewe pamoja na Mawaziri wako walio Waadilifu na Uzalendo katika Utekelwzaji na Mwamko wa Nini Taifa letu linahitaji..na vipi tunayo mikakati ya kuweza kufikia lengo. (Maendeleo ya Taifa) Vyama na siasa tuwaachie wanaojiita wanasiasa...Tanzania haito jengwa na wanasiasa ajili siasa ni Malumbano na Ubishi na mwisho wa siku hakuna uamuzi wala la maana ila litaendelezwa siku ya pili. na likipata washabiki ndiyo itakuwa mada na skendo na magazeti na vijiwe kuka na kuleta Rai sizizo kuwa na mpango na mwisho wake ni UVIVU.. kinachofatia ni ukosefu wa nidhamu na malalamiko yasiyo na mshiko mfano ni wa LAIVU NOT LAIVU..Lakini leo viongozi wa nchi zingine wana waadmire nyinyi viongozi wetu.. Sifa Ya JPJM nchi za nje huwezi kufananisha na Viongozi wa sasa Barani kwetu..Sifa si yakawaida... wanamuona ni kiongozi aliye amua kuwatumikia watu wake kwa hali na mali bila TAMAA...na kweli hana Rafiki aliye Mbadhirifu na anawapiga vita mpaka wajirudi kwamba Tanzania itajengwa na Mtanzania.. Kinachotakiwa ni kuwa rai MWAMINIFU / MCHAPA KAZI / NA MUADILIFU / NA ASIYE NA TAMAA... MUNGU AKULINDENI NA MAADUI KWA UNADUI WAO..MUNGU IBARIKI NCHI YETU NA WATU WAKE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad