Mashindano ya Big Brother Africa yavunjwa

Kama ulikuwa unasubiria kuona mashindano ya Big Brother Africa basi pole sana sababu kwa mwaka huu hayatakuwepo.


Mashindano ya Big Brother yametokea kuwavutia watu wengi kutokana na kukutanisha washiriki wanaotoka mataifa mbalimbali ya Afrila, huku Tanzania ikionekana kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

Taarifa zilizotolewa na waandaaji wa mashindano hayo kupitia M-Net wamesema kwa sasa wanajiandaa kuweka mikakati ili kuboresha mashindano hayo hapo mwakani.


“We wish to thank Big Brother Africa fans far and wide for their continues support over the past edition and promise that the shw will go on, on Dstv, with new and excting productions in store from M-Net,” wamesema.

Mpaka sasa taji hilo la Big Brother linashikiliwa na Idris Sultani aliyefanikiwa kushinda mwaka jana na kupata zawadi ya fedha kiasi cha dola laki tatu.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sasa hiyo ndo mashindano kufutwa? Juu mwaandika vingine ndani vingine..Ngoja niwapeni Ushauri wa bure..Unajuwa mkizoeleka ktk ku anounce uongo kisha watu watakuzoeeni kwa hali hiyo ya kusema uongo. .Kisha mtaandika siku moja habari ya kweli kisha watu wadhanie uongo wa kila siku..mtakimbiwa..siku zote ukweli ndo unakimbiliwa hata kama hauna maana

    ReplyDelete
  2. Lunga gongana next kama hamjaelewa waulizeni watu wawatafisirie.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad