Mashine "iliyotumbuliwa" na JPM Uwanja wa Ndege Imepona na Inafanya kazi Kwa Ufasaha

Hatimaye mashine iliyotembelewa na Rais JPM jana na kukutwa ikiwa mbovu au haifanyi kazi kwa ufanisi sasa inapiga mzigo kama kawaida na ikiwa chini ya uangalizi wa Maafisa Usalama wa Mamalaka ya Viwanja vya Ndege,Polisi na Afisa wa TRA.

Mashine hiyo aina ya Rapscan inayotumika kukaguwa mizigo ya abiria wanaoingia Dsm kutoka Znz,na mikoa mingine ya Tanzania,mapori ya Utalii kama Selous,Mikumi,Sadani na Ruaha pamoja na wasafiri wa nje ya nchi.Ikumbukwe kuwa palikuwa na "uzembe" wa abiria wanaoingia nchini kupitia eneo la TB One,uwanja wa Terminal One una "Status" ya "General Aviation" kwa maana huruhusu kutua ndege za abiria,mizigo na kukodishwa,ambazo zinaweza kuwa za kutoka ndani ya nchi au nje ya nchi

Kwa maana hiyo,Arrival ya Terminal One ni tofauti na ile ya Terminal Two,sababu ya Teeminal Two imegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni "Domestic Arrival" na "International Arrival",hivyo ndege nyingi za domestic katika Terminal Two mizigo ya abiria haina haja kukaguliwa sababu watu wanatoka mkoa mmoja ndani ya nchi kwenda mkoa mwingine,na wale wanaotoka nje ya nchi hawachanganyikani na wa ndani ya nchi

Uwanja wa Terminal One "Arrival" hiyo hiyo moja hutumika na abiria wa kutoka Zanzibar,Mikoani,Mbuga za Wanyama(Porini) na nje ya nchi.Hivyo kuwa na Mashine mbovu eneo la Arrival ambayo inahudumia watu wanaopita toka Zanzibar(Wakiwa na mizigo ya kibiashara kwa nia ya kukwepa ushuru) na nje ya nchi ni "kosa" kiutendaji.Wapo watu kama Pasco wa JF wanaodhani JPM kakurupuka,wasijuwe kuwa "status" ya Terminal One Arrival sio kama ile ya "Domestic Terminal Two"

Vijana wa JPM,hatumpi vitu vya kukurupuka,anapewa data zilizoshiba,ndio maana akifika anaenda moja kwa moja.Jana baada ya kuongea tu kufika saa kumi mashine zikawa zimetengenezwa na mizigo inakaguliwa kwa ufanisi mkubwa.Simu nyingi zilizokuwa zinapitishwa kinyemela toka Dubai via Zanzibar kuja Dsm zimeanza kunaswa,mali pori zisizo na vibari zinaonekana na hivyo kuwa na uhakika wa kutambua nini na nini kinaingia nchini.

Kwa taarifa tu ni kuwa Wamiliki wengi wa ndege Terminal One ni wafanyabiashara wa uwindaji na utalii,matengenezo ya ndege zao hufanyika nje ya nchi,hivyo hufanya udanganyifu wa kwenda porini na kubeba mali pori,kurudi Dsm bila kuushusha mzigo,na baadae kusafiri kwenda nje ya nchi na mzigo "kimyakimya",na wakati ndege zikirudi toka nje huja na bidhaa ambazo ni "dutable",na baadae kuingia nchini bila kutozwa kodi

Ujanja mwingine uliokuwa unatumika na wafanyabiashara wengi ni kushusha mzigo Zanzibar na baadae kuuleta Dsm na ndege za Charter na hivyo kukwepa kosi,Ndege ya Qatar na Oman Air hutua Zanzibar,hivyo wafanyabiashara wengi huja na bidhaa na kuzishusha Znz na baadae wanakuja kama abiria kupitia Terminal One na hivyo kuingiza nchini bidhaa nyingi bila kulipa kodi,kwa mashine ile kutokutumika vizuri basi Taifa limepoteza mapato mengi kwa muda mrefu

JPM kwenda pale jana hajakurupuka,ni matokeo ya jitihada za kumuonyesha sehemu ambapo kuna mianya ya ukwepaji kodi.., Twende JPM ipo siku watakuelewa,hasa utakapoanza kuiachia hela unayoikusanya sasa,wacha tule ugali dagaa kwa muda..Msosi wa uhakika mezani unakuja

By Barafu
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hmmmmmmmm yetu macho na kiini macho

    ReplyDelete
  2. Wakaguzi wa mizigo cargo na bandarini nao ni majipu, nitapeleka umbea kwa bwana magufuli

    ReplyDelete
  3. Hilo li pasco la jf ni liropokaji jmn....kila kitu linapinga mh rais asifanye hv huyo keshapayuka mh kakosea we kipi chema mh rais ameshafanya ukaona sawa....khaa gubu ka kitu gani....nina mashaka familia yako imekumbwa na kadhia ya kutumbuliwa na jpm ndo maana una hasira na mhe.rais...utaisoma namba...

    ReplyDelete
  4. Hapo hakuna cha kushangaa mdau serikali kama haiingizi mapato/ushuru inavyotakiwa unafikiri shule hospitali madawa barabara na kadhalika vitaendeshwa vipi bila ya pesa?Ndio maana kulipa ushuru serikalini ni kitu muhimu sana kwa maendeleo ya nchi pole pole mtaisoma namba na kumuelewa JPM kuna ana nia nzuri na wananchi wake kwa ujumla

    ReplyDelete
  5. Asante kwa taarifa,hiyo nchi ilikuwa shamba la bibi alafu jiulize yule raisi mkwele miaka yote watu wanapiga hela yeye anachekacheka tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Heli wewe umelijua hilo na umenena, yule mkwele alikuwa nizigo na shidaaa kwa mustakabali wa Taifa, ndio maana kila kitu kilikuwa kinaenda shagala bagala, shule za hovyo kayumba, hospital madawa hakuna, wagonjwa wanalazwa chini, hao wakina mama huko kwa kujifungulia ni shidaaa ni kurundikwa tu. Na vifaaa hamna looo haya mataifa yetu ya Afrika yanatia mpka aibu.

      Delete
  6. Majipu mengine yasiwe ya kupandikiza jamani
    naskia mashine zimepona kulikoni???????????????????????

    ReplyDelete
  7. Kazi za mawazili hazijulikani, maana kila siku Ni jpm kutembelea sehemu mbali mbali

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad