Mauaji ya Kutisha Kaole Bagamoyo Jana Jioni..Mama na Mtoto Wachinjwa Kama Kuku

Samahani kwa Kuficha Picha , Sio Nzuri
Watu wawili mama na mtoto wamenyongwa hadi kufa kisha kuchinjwa kama kuku maeneo ya kaole jion ya jana

Habari kutoka Kaole; Majira ya saa 12 jioni jana, ilipita pikipiki eneo hilo ikiwa imepakiza watu watatu, dereva wa nne! Wanaume wawili, mwanamke na mtoto.
Walipofika eneo la darajani, porini kidogo, pikipiki ilipaki, watu wote wakashuka ndipo hatua za utekelezaji mauaji hayo zilianza.

Inadaiwa kwamba, Mama na mtoto wake walinyongwa Kwanza kabla ya kuchinjwa shingoni mithili ya kuku!
Lakini wakati mauaji hayo yakitekelezwa kulisikika makelele porini ambapo baadhi ya wananchi waliyoyasikia walielekea huko ndipo walipokutana na wauaji hao wakiwa na majambia yaliyoloa damu wakitokea porini.

Walipowaona watu hao walikimbia na kuacha pikipiki yao ambayo inashikiliwa Polisi. Katika eneo la tukio, mbali na pikipiki pia kulikutwa simu tatu za mkononi na mkoba wa mwanamke aliyeuawa.
Kwa mujibu wa taarifa, watu hao ni wageni Kaole na mpaka sasa bado miili yao haijatambuliwa!

Picha zinatish mno ndo maana hazijatumwa humu kama una ndugu yako mwenye mtoto wa kiume umri miaka 3-5 halafu kapotea mazingira ya kutatanisha jitahidi kufwatilia
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Walaaniwe jamn walaaniwe nasema hao wauaji Mungu walaani shusha mkono wako wenye hasira waponde wape mateso na wao wafe kwa mateso yani hadi natetemeka

    ReplyDelete
  2. DAH WATANZANIA JAMANI TUMEKUWA WANYAMA KULIKO WANYAMA!!!!MUNGU AWAREHEME MAREHEMU.

    ReplyDelete
  3. hao wauaji wakamatwe na wachukuliwe hatua kali za kishelia wahumiwe hukumu kama waliyoifanya. R.I.P

    ReplyDelete
  4. nimeogopa mno duh walikosa nini huyo mtoto naye amekosa nini??? we baba wa mtoto uko wapi au ni wewe???

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad