Mbio za Mwenge: Kudorora Kwa Ukimbizwaji Kipi Kifanyike ?

Nimezoea kuona mbio za mwenge ambazo zimesheheni shamra shamra, vifijo, sanaa na ujumbe kufikishwa kwa wananchi katika uzito unaostahili.

Mbio za Mwenge za safari hii zimengia Zanzibar kimya kimya na uwepo kwa mbio hizo umepoteza haiba, na hamu hata huwezi kuufuatilia.

Mara ya kwanza kusikia habari zake kuwa umeingia Visiwani ni kupitia ZBCTV wakati Kiongozi wa mbio hizo Nd. George Watson alipotoa misaada ya "vitanda vya kamba ( Mayowe)" maarufu vya kukoshea maiti, kwa Wizara ya Afya, Pemba, kwa ajili ya wagonjwa!

Mbio hizo za Mwenge sasa ziko Unguja ambazo pia zimekosa mvuto na umaarufu na kugeuka kuwa mbio za wanasiasa na askari wateule wachache wa FFU.

Msafara wa jeneza (msiba)unaonekana kukusanya watu wengi kuliko ushiriki wa watu kwenye mbio za Mwenge ( furaha).Kulikoni? Tujiulize, Bado una tija, kuhitajika na thamani kwa wananchi? Kipi kifanyike kurudisha ari, mshawasha wa kuupokea na kuuengaenga kama zamani. Au hili linatokea visiwani tu kwenye watu waliokwisha kata tamaa?

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mwenge uweke makumbusho, anayetaka kuuon awe anauona huko. ni sehemu ya udhaifu wetu kama nchi ila tukubali uishe.

    ReplyDelete
  2. Bwana nassoro mola akuongoze kwa kuanika ukweli,huo mwenge ni ibada toskwa wanaoushabikia!

    ReplyDelete
  3. Tanzania ni ya vyama vingi cha ajabu kila mwaka ni watu wa CCM tu ndo waongozaji wa mwenge
    pili hauna tija kwa watanzania ni tija kwa CCM tu

    ReplyDelete
  4. MWENGE NI JIPU LENYE MATAWI TANZANIA NZIMA
    HATULITAKI HILI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad