Mbunge wa CCM Anusurika Kupigwa na Wabunge wa UKAWA

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Jackline Msongozi juzi jioni alinusurika kipigo kutoka kwa wabunge wanawake wa UKAWA baada ya kuwaeleza kuwa upande huo una wabunge wawili tu wenye michango ya maana ambao ni Upendo Peneza (Viti Maalumu Chadema) na Magdalena Sakaya (Kaliua - CUF).

Akichangia mjadala wa bajeti kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Msongozi aliishambulia kambi ya upinzani akieleza kuwa kuna mlevi mmoja amechangia upande wa upinzani kuhusu uuzwaji wa nyumba za Serikali wakati waliohusika na uuzwaji huo wamehamia upinzani ambao ni Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Msongozi alisema hakuna mke mwenza anayeweza kumsifia mwenzake, hivyo upinzani hauwezi kuisifia CCM kutokana na kazi wanayoifanya.

Baada ya kusema maneno hayo na wabunge wengine kuchangia, Bunge lilipoahirishwa wabunge wanawake wa upinzani wakiongozwa na Sabrina Sungura na Ester Matiko walimfuata Msongozi wakitaka kumshambulia, lakini aliondoka moja kwa moja pasipo kusimama popote.

Sungura alipoulizwa alisema kuwa mbunge huyo angesimama wangemshughulikia
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndio wabunge wa TZ yetu hao ni taabu hat kujua eti tuliwachagua mhh
    Utumbo mtupu na utoto
    Hawa si wana siasa ila wanafanya siasa kama ajira tu hawajui lolote

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad