Mbunge wa Ulanga, Godluck Mlinga (CCM) Atoa Tuhuma nzito kwa TRA, TCRA, EWURA

Mbunge wa Ulanga, Godluck Mlinga (CCM) ameyatuhumu mashirika ya umma ambayo hayajajiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuwa watendaji wake wakuu wamepewa malipo ya asilimia 10 ili mashirika hayo yajiunge na kampuni binafsi za bima.

Ameyataja baadhi ya mashirika hayo ya umma yaliyokaidi kujiunga na NHIF licha ya kulazimishwa kisheria kuwa ni Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Yapo mashirika ya umma yanakataa kujiunga na NHIF wakati sisi wabunge tumejiunga, wao ni nani? Wakubwa wao wanapata asilimia 10 na wanajiunga na kampuni za bima ya afya binafsi…

“Mimi niliwahi kuwa Compliance Officer wa NHIF nikaenda TRA, nikawaeleza umuhimu wa kujiunga NHIF unachangia pesa kidogo unapata huduma nyingi lakini bosi wao akanijibu pesa si tatizo na afadhali ametumbuliwa huyo bosi wao, yule angekuwa ofisini kwangu asingetoka,” alisema Mlinga na kuongeza:

“Kila sehemu wananitaja Mlinga Mlinga, napata vitisho vingi lakini serikali inanilinda na kama jeshi (JWTZ) limeweza kusambaratisha M23 itashindwa kunilinda mimi…wengine wananiita teja hivi teja anavaa suti iliyonyooka kama mimi, siwezi kukasirika kwa sababu si kweli lakini wangeniita mbilikimo ningekasirika kwa sababu kweli.”

Mbunge huyo alitaka serikali ikomeshe tabia ya wanaume kubaka wazee na kufafanua “najiuliza wanawake wa mikoa yenye ubakaji wa wazee ni wagumu kuelewa hadi wazee wabakwe?”

Naye Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby (CCM) amesema sasa ataanza kuacha kuwashawishi wananchi wake kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kutokana na mfuko huo kutopeleka dawa na chanjo za watoto kwenye vituo vya afya, badala yake inapeleka kondomu na vifaa visivyo muhimu kwa wananchi.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ropoka sana Magufuli hakupi uwaziri ngoooooooooooooooooooooooo

    ReplyDelete
  2. Milinga!! Kidogo umenichanganya..umetaja Jeshi na kulisifia utensaji wake na umejigamba on personal protection. PIA umetuhadharisha kwamba Una mnadui wengi wanakkutafuta..na unatutaarifu Kuwa watu wana dhana ya wewe kuwa tena..lkini Kafika mavazi u ayo vaa haya dhihirishi hiyyo dhama kwa ajili wewe Ni msafi kwa muonekano Wako..pia umejaribu kutuambia kwamba wakosa maadili Wako wengi Kafika Taifa letu na wanashindwa Kula na hatima yake wanawakamata Bibi zetu we umuri WA mmguu kaburini na serikali haijalifanyia kazi ya kustahili Kafika ukomeshaji na PIA umenaribu kutupa CV yako ya nini ulichokuwa ukifanya kabla na umejaribu kuleta masaa ya kuwa Rushwa na Ubadhirifu bado ikoo na watendaji wakuu baadhi ya taasi za serikali Ni wafaidika wakuu..Je Nimekuelewa hivyo au Una ajenda ilijificha..Umenichanganya..ILA KAMA ULICHUKUA MUDA KATIKA BUNGE LETU KUSIMAMA NA HAYA NDIYO UCHANGIAJI WAKO.. HHAPO CHA MAENDELEO SIKIONI..JE WA DIZAINI MKO WENGI???!! NDIYO TUNARUDI KKULE KULE.. MIMI NIKO RADHI KUWAFANYIA TATHMINI NA MKOSA MADA YA KULETA BUNGENI AANZE MIMI HIVI..HUYU VILE..NA HAWA HIVI NA WALE VILE..TUMRUDISHE KWA CHINUA ACHEBE ( Things Fall Apart) jamani tuna majukumu waliyo tukabidhi wananchi na wanatusikiliza..LAIVU HATA KATIKA KIPINDI MAALUM..SI TUNAJUA HILO...

    ReplyDelete
  3. Mlinga Seems you did try to sell the Service..Guess what happened. You have not been an effective salesman OR the approach was not right 👉..I recommend and suggest that you need further training to enhance your skills and abilities..believe me once you have these..will take you to next level. Huu Ni ushauri wangu kwa lakini usimame na kutuletea hadithi ndefu hatuambbulii kitu tunataka actin/ performance / achievement ili tuijenge kimaendeleo na kwa muda mfupi Tanzania yetu na hii awamu yetu ya tank hatutaki wappiga filimi nyingi..wote Ni wavivu..nakuomba usiwe mmoja katika hao bidiika na wajibika..JP anatuangalia na kutufatilia tusimwongeze kazi zaidi.. Ana mengi ya maa a zaidi ya kufanya..Asante kwa uelewa Wako na ushiriki Wako katika vikao vyetu hapa Dodoma..Hapa Ni kazi tuu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad