Mch. Peter Msigwa, kwa Mahojiano ya ITV Jana Umechemka

Kama vile amesahu ahadi za Ukawa kutoa elimu bure kuanzia Darasa la kwanza hadi chuo kikuu. Jana Msigwa alipinga vikali swala la elimu bure huku akipata kigugumizi kujibu kwa ufasaha Maswali ya Muandishi wa ITV. Kwa hili kweli kabisa Mimi nimekushusha kabisa kwasababu Muitikio wa elimu bure ni mkubwa sana na kila mtu anafaidi keki ya Taifa kupitia hili la elimu bure na bila shaka ni jambo bora kabisa kumpa mtoto wa kitanzania elimu.

Pili ni kupinga swala ya Kubana matumizi hasa kutotumia hela kwenye sherehe na kuzielekeza kwenye Maendeleo ni jambo jema kabisa kila mtu analisapoti kasoro wewe tu Mtumishi. Magufuli anania ya dhati kuua Siasa za kuropoka ropoka . Zije siasa za watu wabunifu kama Professa J maneno machache vitendo vingi.

By Pascal Ndege

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuhubiri kwenye nyumba za ibada kunatofautiana sana na mambo ya siasa.

    ReplyDelete
  2. Wakichaguliwa na kushinda uchaguzi basi vichwani mwao wanamaindi kuiba na kujenga maghorofa yao fake na kushindana kununua magari ya kifahari na kusahau ahadi zote "hewa"walizokuwa wanawa promise wananchi katika vitongoji vyao ili wapewe kura na hiyo kura hugeuka na kuwa "kula"kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho ipo siku mtanyooka nyinyi wote wenye tabia ya wizi na ahadi zenu potofu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad