Mimi Sifanyi Mapenzi, Hata Boyfriend Wangu Anajua Sipendi Kufanya Mapenzi – Gigy Money

Video queen ambaye haishiwi vituko, Gigy Money amefunguka kwa kusema kuwa yeye siyo mtu wa kupenda kufanya mapenzi kama watu wanavyodhani.


Akizungumza na Bongo5, Gigy amesema maisha aliyopitia yamemfanya awe ni mwanamke asiyependa kufanya mapenzi.

“Mimi nimepoteza ile ari ya kufanya mapenzi au kuwa na mpenzi mmoja au nijiachie na mwanaume kama mtu na mpenzi wake siwezi, sasa hivi natafuta maisha, pesa mbele,” alisema Gigy. “Kama yeye ana wivu na mimi, mimi sina wivu na mwanaume,”

Gigy amesema taarifa za kwenye mitandao ya kijamii kwamba anajiuza siyo za kweli, kwani yeye ana mwanaume ambaye anamuudumia kila kitu ingawa hawafanyi mapenzi.

“Nina mtu ambaye ananihudumia, ananipa mtaji ya biashara zangu. Pia hata kwenye muziki anawekeza pesa yake. Kwa hiyo waache wanifikie hivyo wanavyofikiria, mimi nafikiria navyojijua, mimi nipo tofauti sana na wanavyozungumza, ukijaribu kukaa na watu wangu wa karibu watakwambia,” alisema Gigy.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuna mwanaume anakuhudumia alafu umpi kitumbua chako?wadanganye hao hao.

    ReplyDelete
  2. Huoni hata aibu mtoto wa kike "hufanyi mapenzi"na hizo picha zako unazoziweka mtandaoni na hiyo mikaaji yako ya kama bata anataka kunaniii.... mmmmmh....yaani ni vitu viwili tofauti kabisa kumbuka kuwa mla vya watu na vyake lazima viliwe au mikono miwili hujiosha kwa zamu

    ReplyDelete
  3. muongo wewe nani atakupa mtaji bila kulala na wewe, hata wanawake wanaofanya mapenzi na boyfriend zao hawapewi mtaji unamdanganya nani

    ReplyDelete
  4. Ikiwa hayo maneno yako ni kweli, basi huyo mwanaume wako ni bwege. Akupe mtaji halafu hayo makalio unayoyaanika wafaidi wengine

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad