Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania limeguswa na hujuma kwa Rais Magufuli

Mei 8 2016 Jukwaa huru la Wazalendo Tanzania limekutana na Waandishi wa Habari Dodoma ili kutoa tamko lao kuhusu hujuma dhidi ya Rais John Pombe Magufuli.

Katibu wa jukwaa hilo Mtela Mwampamba amesema
’Kwa miaka mingi Watanzania tumekuwa tukipiga kelele tukilia juu ya kero mbalimbali za Serikali kushindwa kupambana na watumishi wasio wema na wabadhirifu, mafisadi, wala rushwa na wahujumu uchumi‘

‘Vita hii tumekuwa tukipigana sisi wanyonge na baadaye ikaungwa mkono na makundi mbalimbali wakiwemo wanasiasa, Sasa tumempata Rais Magufuli anayefanya kazi bila kuchoka kuifikisha Tanzania tunakokutaka, wanasiasa hao wamegeuka na wanaanza kumhujumu‘

‘Tumeshangazwa zaidi tunaposoma na kusikia katika vyombo vya habari baadhi ya wanasiasa wakianza kumkejeli Rais Magufuli eti anaendesha nchi kinyume cha sheria na kuipeleka katika utawala wa kiimla‘

‘Ni kwasababu hii, sisi wazalendo tunasema hoja za wanasiasa na wasomi kusema Rais analeta utawala wa kidikteta kwa kutumbua majipu tunaona ni hali zilizojaa hisia binafsi na zaidi ujasiri wa hujuma‘

Mwampamba hajaacha lipite hili la Sukari, nalo anasema…>>’Baadhi ya wafanyabiashara kuficha badhaa muhimu ya sukari, tunatumia fursa hii kuwakumbusha kuwa waachane na hujuma hiyo mara moja.‘

‘Wanaoendesha uhujumu huo wa uchumi ni sawa na hawa wanasiasa wanaoendekeza hujuma dhidi ya Rais Magufuli ili asiendeleze mageuzi ambayo Watanzania wenyewe waliyataka na wameyasubiri kwa muda mrefu‘
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Waseme wasemavyo...WE have Mandated JPJM due to his dedication and Passion combined with Leadership skills and chosen style.. More over We deem him as a game changer in Africanleadrship... Many world leaders are admirer OF our JPJM and are keen to follow his footsteps and revamp their leadership Skills and Corruption riden countries.. OUR IS A SAVIOUR OF A COMMOM MAN BY COMMON MAN... MUNGU ATULIDIE NA AMUONOSHEE MAADUI NA UADUI WAO JUU YAKE... JP ENDELEA BILA KUONA HAYA NA HATUYATAKI HAYA WAZEMBE KIBOKO YAO JPJM

    ReplyDelete
  2. Waseme wasemavyo...WE have Mandated JPJM due to his dedication and Passion to Lead combined with his Leadership skills and his unmatched chosen style.. Moreover He is a Game Changer in Africanleadrship... Many world leaders are admiring him (Dr JPJM) on his Dedication to serve the Nation and are keen to follow his footsteps and revamp their leadership Skills and Corruption riden countries..Magufuli IS OUR SAVIOUR OF A COMMOM MAN BY COMMON MAN... MUNGU AMULIDIE NA AMUONDOSHEE MAADUI NA UADUI WAO JUU YAKE... JP ENDELEA BILA KUONA HAYA NA HATUYATAKI HAYA WAZEMBE KIBOKO YAO JPJM.. wadharirifu si rafiki zake Wala hali nao Sahani Moja... KAMAGULI NI KATOTO CHETU WENYE... NA HATO TUANGUSHA..... ENDELEA BABA MWEZI MTUFUKU PIA UKO KARIBU ...HII NI FUNGA YA MWANZO KATI UONGOZI WAKO.. TUOMBE SALAMA NA MUNGU AIBARIKI NCHI YETU NA AKUBARIKI WEWE PIA.. NA AKUPE UMURI UHUDHURIE BARAZA LA IDDI....

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad