Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Awakemea Wafanyabiashara wa Sukari Wanaompigia Simu Usiku Kutaka Kumpooza

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amefichua kuwa amekuwa akipigiwa simu na baadhi ya wafanyabiashara vigogo wenye nia ya kutaka kupunguza makali ya operesheni inayofanywa na wilaya yake dhidi ya waficha sukari.

Kwamba simu hizo amekuwa akipigiwa hadi usiku wa manane na huku wengine wakimtumia ujumbe mfupi wa simu wa maandishi (SMS). Amekemea wafanyabiashara hao na kutaka waache mara moja mchezo huo, kwani vyombo vya dola vinaendelea kuwafuatilia.

Hapi alisema hayo jana wakati akizungumzia suala la Uadilifu kwenye Mkutano wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wanaotokana na shirikisho hilo.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya alibainisha kwamba amekuwa hapokei simu hizo na SMS hizo za wafanyabiashara wakubwa kutokana na sababu mbalimbali.

“Sababu ya kwanza sina sababu ya kuzipokea, lakini pili nahofia nikizipokea nitarekodiwa na wafanyabiashara hao na sauti yangu itasambazwa kwenye mitandao, kuonesha nipo pamoja nao.

“Wakati mwingine mpaka usiku wa manane wanapiga simu na kutuma meseji na wengine wanajitambulisha. Lakini huwa namuonyesha mke wangu na kumwambia sina sababu ya kuzipokea, kwani naweza nikapokea lakini katika mazungumzo yetu nikasema neno ‘sawa’, kisha neno hilo linaweza kusambazwa katika mitandao kuonyesha kwamba nia yetu ni moja ya kuficha sukari”, alisema Hapi.

Alisema hao wafanyabiashara wanaoficha sukari, wanaleta madhara makubwa kwa jamii na uchumi wa nchi, kama vile kuua viwanda vya sukari nchini.

Alisema wafanyabiashara hao wamekuwa wakiweka ‘oda’ katika viwanda vya sukari kuchukua bidhaa hiyo, lakini hawaendi kuichukua kwa madai ya kwenda kuichukua siku za baadaye, lengo likiwa kuificha.

Hapi aliwaomba wakazi wa wilaya ya Kinondoni, kuendelea kuisaidia serikali kufichua watu wote walioficha sukari.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kijana punguza sifa fanya kazi media hazikusaidii mbona wenzako WA ilala na temeke wanapiga kazi bila kujionesha onesha kwa media

    ReplyDelete
  2. Mh Rais akikuomba utaje majina ya hao wanaokupigia utawataja? Kama kweli upo katika kupigania maendeleo na kuwakomesha hao watu kwanini usitoe report police ukapokea simu zao na kuwasikiliza huku mkiwarecord s wanachotaka? Ili kulikomboa Taifa? Sikia kijana hujachaguliwa kufanya comedy mambo ya kuvaa kimgambo kuropoka hovyo watanzania hatupendi kazi haifanywi kwa vyombo vya habari mngekuwa mnathamini vyombo vya habari mngewaacha waonyeshe bunge live.. fanya kazi tuone maendeleo acha vituko eti mke wangu huwa namuonyesha sasa sisi mkeo ni nani kwetu? Mama wa wilaya ya kinondoni au? Fanya kazi acha maneno.

    ReplyDelete
  3. mheshimiwa, unaweza kuwataja hao watoa rushwa? au iikiwezekana peleka majina/namba zao takukuru.

    ReplyDelete
  4. Huyu nae anautafuta ukuu wa mkoa kwa nguvu.

    ReplyDelete
  5. Tatizo wanateuliwa kichama hamna mtu hapo Ni maonesho tuu

    ReplyDelete
  6. Wewe umechaguliwa umma wa watu wakijua ni mzalendo na mtu uijuaye sheria ya nchi - hapo kwako wewe ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama chini yako unaye PCCB, Polisi na Usalama sasa kwani huwatumii kukamata hao wakushawishio.

    Tuache kusaka sifa nyepesi - tumia vyombo vya usalama kuwajibisha watoa rushwa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad