Mose Iyobo asema kuwa na mahusiano ya mapenzi na Aunt Ezekiel kumemsaidia sana

Dancer wa Diamond, Mose Iyobo amesema kuingia kwenye mahusiano ya mapenzi na Aunt Ezekiel kumemsaidia mambo mengi katika maisha yake.
Aunt na Mose

Akizungumza na Bongo5, Mose amesema hasa hasa amenufaika sana na umaarufu wa Aunt Ezekiel ambae ni staa mkubwa katika tasnia ya filamu.

“Kuwa na mahusiano na mama Cookie kumenisogeza sana,” alisema Mose. “Kwa sababu ni star wa filamu toka kitambo sana. Mimi nilikuwa najulikana lakini siyo kivile, lakini nilivyokutana na Mama Cookie kuna vitu vingi vimeongezeka katika maisha yangu,” alisema Mose.

Pia Mose amesema mwanae Cookie ataonyeshwa hadharani rasmi kwa mara ya kwanza tarehe 21 mwezi huu baada ya kutimiza mwaka mmoja

Chanzo:Bongo5

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad