Mrembo Anayedaiwa Kutoka Kimapenzi na Mwanamuziki Diamond Afunguka

Mrembo huyo aliyeuza nyago kwenye Video ya Wimbo wa Kwetu wa msanii wa Diamond, Irene’ Lynn’.

Mrembo ambaye wiki mbili zilizopita aligeuka gumzo baada ya kudaiwa ‘kuchepuka’ na staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Irene’ Lynn’ kisha kuleta mtikisiko kwa mpenzi wa msanii huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ amefunguka kuhusu ishu hiyo.


Akizungumza wikiendi iliyopita baada ya kubanwa aseme ukweli kama anatoka kimapenzi na Diamond, mrembo huyo aliyeuza nyago kwenye Video ya Wimbo wa Kwetu wa msanii wa Diamond aitwaye Raymond alisema kuwa hata yeye ishu hiyo inamshangaza.


 Irene alisema siku zote watu hawajiamini wanapomuona msichana mzuri akifanya kazi na mtu fulani na mara nyingine humwekea wivu na kuibua mambo mengine. Irene aliweka wazi kuwa kilichompeleka Wasafi ni kufanya kazi ya Wimbo wa Raymond na hakuna kingine kilichoendelea.

“Mkataba wangu na Diamond uliisha baada tu ya kufanya video ya msanii wake,” alisema Irene. Mrembo huyo alitiririka kuwa ishu hiyo inamtesa na kumsumbua kwa sababu watu wengi wanajua kuwa ni kweli ametembea na Diamond, jambo ambalo si kweli.

 Skendo ya Irene kutembea na Diamond ilileta mtafaruku mkubwa kwenye familia ya mwanamuziki huyo kiasi cha dada wa mwanamuziki huyo, Esma Platnumz, kuingia kwenye mgogoro mzito na Zari ikielezwa kuwa mrembo huyo ni rafiki yake na alijua kilichokuwa kikiendelea.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. unafikiri atasema nn. toa funza kichwani

    ReplyDelete
  2. Do ndo fiada ya kutembea na DOMO
    wanaume wote duniani utembee na DOMO kwa lipi
    umaarufu huna tena
    fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  3. Domo ndo alomtongoza kwa nini akatae na yeye anataka kuingia kwenye giness bok

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nafikiri uliteleza kimaandishi kidogo ulimaanisha"GUINNESS BOOK"Mdau au?

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad