Msamaha wa Jakaya Kwa Baadhi ya Watuhumiwa wa Ufisadi wa EPA Waleta Utata

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete hakutumia ibara ya 45 ya Katiba kutoa msamaha kwa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), wanaoelezwa kuamriwa kurejesha fedha walizochukua.Aidha, alisema pale ambapo kuna makosa, Rais anaweza kumsamehe mtu ambaye tayari amehukumiwa au kupewa adhabu kwa kutumia ibara hiyo.Alisema, “Mimi kwa taarifa nilizonazo Mheshimiwa Rais mstaafu hakutumia kifungu hicho,” Dk Mwakyembe alisema bila kueleza kifungu kilichotumiwa.Alisema hivyo jana bungeni mjini hapa, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji (CUF) aliyetaka kujua endapo Rais aliyepita alitumia madaraka yake vibaya, alikosea au alikuwa sahihi kuruhusu baadhi ya watuhumiwa walipe fedha walizodaiwa kuzifanyia ubadhirifu kupitia akaunti ya EPA (Hawakutajwa).Pia, mbunge huyo katika swali lake la pili la nyongeza alitaka kujua ni lini watafikishwa mahakamani akieleza kuwa msamaha waliopewa haukuwa wa kikatiba na kwamba wanastahili kushitakiwa.Katika swali lake la msingi, Haji alitaka kujua iwapo Rais ana mamlaka ya kisheria kutoa msamaha kwa watuhumiwa wa uhalifu wa aina yoyote ambayo mashauri yake yapo katika vyombo vya dola kwenye hatua za uchunguzi, upelelezi au mahakamani.


Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ki ukweli hana.inakingana na sheria za nchi. Hii inaonyesha wazi yeye ni mfugaji wa watu hao. Ni kiongozi inabidi atazamwe kwa ukaribu mno.matatizo mengi yametokea chini ya utawala wake. Na bado anayatetea kwa kuwapa msamaha. Ni watu wlio na ukaribu sana naye, ni watu wa ikulu, watu wa usalama.bado analiweka taifa pabaya ingawa hayupo tena ikulu.anamwekea vikwazo raisi Magufuli kikazi, anavunja sheria, anaweka bunge pabaya na chama chake pabaya zaidi. Kwa nini apewe nguvu mtu mmoja kudoctate nchi.watu wengi Tanzania wanajua yeye ni pingamizi kubwa la mabadiliko nchini.Inabidi akae kando kusudi Raisi wa sasa afanye kazi vipasavyo. Ni pingamizi kuu la maendeleo.mpaka leo bsdo anakumbatia majina ya wauza unga, anacheo kikuubwa ameshindwa kutimiza wajibu wake. Kwani hajui cheo ni dhamana si kwa walanguzi, wezi, wahujumu, wauza unga, wapora ardhi, wauaji wa tembo, na wakuu wa nchi wa nje na mabalozi aliowapa xawadi za meno ya tembo. Kwa maono yangu. Ni hawa watumbuliwe kwanza, bila hivi hii tumbua ya vidagaa haina maana .waescrow ndio wahujumu wakuu, mafini na ubia na makampuni feki chini ya uongoxi wake. Ingekuwa nchi nyingine kwa sasa angekuwa jela kupitisha uchunguxi uende sambamba. Lakini anakuwa pingamizi na influens kubwa ya uchaguxi wa watu wake wabaki serikalini.ameritaya apumxike.apishe njia. Na afanyiwe kazi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad