Najma: Sijali Mpenzi Wangu Baraka Da Price Ametoka na Wangapi Hapa Nahisi Nimefika

Mwanamuziki Najma Dattan ‘Naj’ ameibuka na kusema kuwa kwa msanii mwenzake Baraka Da Prince amefika wala hajali ametoka na wanawake wangapi kwa sababu hata yeye ana ‘pasti’ yake.

Akizungumza na Ijumaa, Najma alisema kuwa amekuwa akiwashangaa wasichana waliopita kwa Baraka ndiyo wanamuongelea kila siku wakidai anakula makombo lakini Baraka mwenyewe haongelei kabisa uhusiano wa watu wake wa zamani.

“Sijali ametoka na wangapi, hayo ni maisha ambayo kila mtu anapitia. Niseme tu kwamba sijawahi kumtambulisha mwanaume kwetu, hapa kwa Baraka nahisi nimefika kwa sababu ndiye mwenye penzi la kweli, kitakachofuata muda si mrefu ni ndoa tu kwani wazazi wetu wanaujua uhusiano wetu,” alisema Najma.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mr Blue hana time yakuangalia show zenu.huyo binti anajua kuact.yaani yote ni kumuonyesha Mr Blue.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad