Nay wa Mitego: Gigy Money Anatafuta Kiki Kwangu

MKALI wa Ngoma ya Saka Hela, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameamua kumfungukia muuza nyago kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kuwa anatafuta kiki kutumia jina lake katika mahojiano anayofanya na vyombo mbalimbali vya habari.

Akichonga na Showbiz Xtra, Nay alisema kuwa amekuwa akisikia juu ya Gigy akimsema si chochote kwake na kwamba ni mbahili alishawahi kumlipa elfu ishirini baada ya kumaliza kutengeneza video zake.


 “Yaani huyo Gigy anatafuta kiki, namshangaa sana kila sehemu kunisema hovyo, kwanza hatuendani kwa chochote,” alisema Nay.

Hivi karibuni katika mahojiano na Global TV Online, Gigy alisikika akimponda Nay kuwa ni mtu bahili na haitakuja kutokea yupo naye iwe kikazi ama vyovyote kwa kuwa hana hadhi ya kuwa naye.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ye gigi anahitaji pesa yake tu.. mlipe basi ili yaishe ndio tutajua kuwa wewe sio bahili. ela zako za mawazo sana inatokana na laana ya kupiga muziki kimajungu. na uwezi kupata tuzo kwa muziki wako.

    ReplyDelete
  2. inasemekana au gigi Money mwenyewe alisema ulimlipa elfu ishirini TU kwenye video yako halafu ukasingizia ana sura mbaya, sasa kama anayo sura mbaya kwa nini ulimuweka katika video yako? Kuwa na adabu na shika adabu yako Ney ndiyo maana demu wako wa Mwanza alilala na wanaume wengine, mlipe hela yake Gigi Money ndiyo atakuacha, inaonekana unaonekaka hauna adabu kwa wasichana wadogo, Ney wa mitego SHIKA ADABU YAKO

    ReplyDelete
  3. nay wa mitego alisema gigi Money ana sura mbaya mimi namuona gigi Money anayo sura nzuri kuliko ney wa mitego hata sura hana pamoja na kujisifia kote ney wa mitego acha kujisifia sura huna hata kidogo na msichana akiwa na wewe utakuwa umemroga si hivi hivi

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad