Nimemuweka Wazi Mpenzi Kupunguza Usumbufu - Ommy Dimpoz

Msanii Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake 'Achia boy' amefunguka na kusema kuwa ameamua kumuweka wazi mpenzi wake ili kupunguza usumbufu kutoka kwa watoto wa kike.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio, Ommy Dimpoz alidai kuwa kufanya hivyo ni kupunguza kasi ya watoto wa kike ambao wamekuwa wakimsumbua na kumtaka kimapenzi.

"Unajua saizi nimeamua kumuweka wazi mpenzi wangu ili wajue yupo na kupunguza usumbufu kwa watoto wa kike ambao wanadhani labda niko single, japo yupo mbali lakini kufanya hivyo inasaidia" alisema Ommy Dimpoz

Mbali na hilo Ommy Dimpoz alisema mpenzi wake huyo kwa sasa anasomea udaktari nchini uingereza na kudai ni mtu wa Afrika Mashariki.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nahissi kama vile unashindana na ile nyimbo shika adabu....

    ReplyDelete
  2. Wadanganye wasiokujua banaaaa

    ReplyDelete
  3. Mwanamuziki mmoja illiterate na demu mmoja msomi anayesomea u-daktari duh!!.....patamu hapo, halafu yuko mbali naye sasa wallaaaaaahhhhh

    ReplyDelete
  4. Huyo naye kaishakuwa Ndi-ndi-ndi-ndi hahahahahaha aaaaaaaahhhhhhhhhh

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad