Rais Magufuli Asema yeye Siyo Katili, Anawatumikia Watanzania ili Kurejesha nchi Kwenye Mstari

Rais John Magufuli amewataka Watanzania wasimuone katili kwa kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji wa Serikali, kwakuwa anataka kuirejesha nchi kwenye mstari.

Akizungumza katika misa ya Jumapili kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Tokeo la Bwana Burka jijini Arusha, Rais Magufuli alisema watu katili ni wale ambao walikuwa wanawaibia Watanzania na kuwanyonya wanyonge.

Dk Magufuli alisema analazimika kuchukua hatua ya kuwafukuza kazi si kwamba ni katili, bali lengo ni kuwatumikia Watanzania na kuirejesha nchi kwenye mstari.

Alisema Tanzania ni taifa tajiri, hakuna sababu ya wananchi kulalamika kila kona, kwani kuna ardhi ya kutosha, madini ya kila aina, wanyama wa aina mbalimbali ambao baadhi wameanza hadi kupelekwa nje.

“Ninapochukua hatua nataka kuweka Tanzania iliyonyooka, mimi tayari nimesema nimejitoa sadaka kwa Watanzania hasa wanyonge,” alisema.

Aliongeza kuwa hatawaangusha Watanzania na hatabadilika, ataendelea kusimama na kutetea haki za Watanzania maskini na siku zote atatembea na maskini.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. KWA MWENDO HUU... NAAMINI KABISA TUTARUDI KWENYE MSTARI NA TUTAJUA WAJIBU WETU KATIKA KULITUMIKIA TAIFA KWA UADILIFU NA KUWA WAKWELI KATIKA MABO YA MAENDELEO YA NCHI.. RUSHWA / UBADHIRIFU / CHUKI / UPENDELEO HIVI VYOTE VITAKUWA NI HISTORIA..KWA KASI HII JPJM MUNGU AKUPE AFYA NA UMURI ULITUMIKIE TAIFA LETU KADIRI UWEZAVYO.. NA KILA ATAKAE KWENDA KINYUME NA MAADILI YA UWAJIBIKAJI.. SISI TUMUWAJIBISHE NA HATOKUWA MWENZETU MAANA YAKE NI MCHELEWESHAJI NA MVIVU...TUNAMKANA WAZI WAZI MCHANA MCHANA... ENDELEA BABA..JPJM

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad