Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Waziri Wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga Baada Ya Kuingia Bungeni Akiwa Amelewa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016.

Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kufuatia kitendo cha Mheshimiwa Charles Kitwanga kuingia bungeni na kujibu swali linaloihusu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

20 Mei, 2016
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. so sad.... wengine wanapata kazi nzuri wanazichezea, huruma sana jamaa pombe tu ndio imekuponza dah! kweli magufuli wewe ni noma la tingatinga! endelea JPJM wengine huku hatuna kazi wengine wanachezea kazi!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad