Rais Magufuli Atetea Uamuzi wake wa Kutimua Wafanyakazi

Rais John Magufuli ametetea uamuzi wake wa kuwatimua baadhi ya watumishi wa umma wanaokiuka maadili akisema anataka kuirejesha nchi kwenye mstari.

Rais amesema hayo leo alipozungumza na waumini katika misa ya Jumapili katika Kanisa Katoliki parokia ya Tokeo la Bwana Burka jijini Arusha.

Amesema watu katili ni wale ambao walikuwa wanawaibia Watanzania na kuwanyonya wanyonge.

Amesema analazimika kuchukua hatua ya kuwafukuza kazi si kwamba ni katili, bali lengo ni kuwatumikia Watanzania na kuirejesha nchi kwenye mstari.

Rais huyo aliyejibatiza “mtumbua majipu”,  amesema Tanzania ni taifa tajiri, hakuna sababu ya wananchi kulalamika kila kona, kwani kuna ardhi ya kutosha, madini ya kila aina, wanyama wa aina mbalimbali ambao baadhi wameanza hadi kupelekwa nje.

"Ninapochukua hatua nataka kuweka Tanzania iliyonyooka, mimi tayari nimesema nimejitoa sadaka kwa watanzania hasa wanyonge," alisema.

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. JPJM...Hivi ni sawa sawa na asiye weza kutufanyia kazi ni Bora yeye mwenyewe aachie kamba..tuna vijana ambao wana upeo mzuri na wausongo wa ajira.. Sasa basi hapa na awamu yetu hii anaye lega lega ...na kutokuwa na Nidhamu na ufanisi wa kazi... NJE ..TENA NJEEEEEEEEEE HALAFU NA WALIOKUWEPO TUNA ANZA JUWAEVALUATE KILA MIEZI MITATU ( MARA NNE KWA MWAKA KUANGALIA PERFORMACE YAO.... BABA UNANIKOSHAAAA... ENDELEA WEWE SASA NDIYO UTAKAE WACHA MISINGI YA BAADA NADHANI TUKICHUKUA HII TABI NI KWAMBA HATUTURUDI NYUMA... ITAKUWA SASA KWENDA MBELE....SIASA NYINGI HATUTAKI TUNATAKA PERFORMING TEAM ASIYE WEZA HII SAFARI SI MWENZETU.... ENDELEA JPJM... TUKO BEGA KWA BEGA.... WABUNGE PIA TUTAWATATHMINI UZEMBE NA POSHO NA UWAJIBIKAJI..WANAFOCUS LAIVU NOT LAIVU...TUSIPOTEZE MUDA WA UJENZI WATAIFA KWA MADAAA ZISIZO NA KICHWA WALA MIGUU...HII YA BUNGE TUMWAACHIE NDUGAI NA KAMATI ZA NIDHAMU BUNGENI...HAYATURIDHISHI LAKINI TUYAFANYIE KAZI....MUNGU AKUPE AFYA NA UMURI TAWILE...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli nimeamini yale maneno aliyekuwa akituambia mwalimu wetu wa kiswahili enzi hizo nilipokuwa nikisoma Tambaza sec/school 1978 kuwa kiswahili ni lugha ngumu sana japo kuwa ni lugha yetu ya taifa sisi watanzania lakini sio tija kabisa shauri huyo ndugu aliyetoa mada yake hapo juu mimi sikumuelewa kabisa anamaanisha nini shauri ameandika kiswahili kibovu ni tabu kumuelewa labda alimaanisha vizuri tu lakini jinsi alivyo kiboronga kiswahili ni kasheshe

      Delete
    2. Kumbe ykijuwa tambaza nie nulikuwa mkwawa .tofayti ya ya amatifone wewe yakwako ipi?? Mie Ile ya kadi mbili

      Delete
    3. Sisi mbona tunamwelewa..Tena Vizuri Sana..ni mchangia nzuri Sana WA Udaku. Na anaelekea msomi nzuri Na mwenye upeo upeo WA huku tunapo elekea Na Ni mkereketwa WA maendeleo ya nchi..jaribu kusoma uchangiaji wake kwa makini

      Delete
    4. Amechangia madaa nzuri tu, tena yenye kueleweka, inayozungumzia mustakhabali wetu wa Taifa. Hongera mchangiaji hapo juu achana na huyo mkosoaji wa lugha. Mbona umeleweka vizuri tu. Maneno mengine ni kutokana na mtelezo wa simu, muda mwengine inabadilisha maneno

      Delete
  2. Si bora huyo anaboronga lugha. Hebu fikiria wengine Wanavurunda Kazi na Wajibu wao..Mie namuelewa hivyo huyo Mdau hapo juu anaonesha ni mpenda Maaendeleo ya Tanzania yetu Mpya...na ni mwenye uwezo akipewa nafasi kama hajapewa..Bwana asifiwe na amtangulie...JP HAPA KAZI TUU

    ReplyDelete
  3. Si bora huyo anaboronga lugha. Hebu fikiria wengine Wanavurunda Kazi na Wajibu wao..Mie namuelewa hivyo huyo Mdau hapo juu anaonesha ni mpenda Maaendeleo ya Tanzania yetu Mpya...na ni mwenye uwezo akipewa nafasi kama hajapewa..Bwana asifiwe na amtangulie...JP HAPA KAZI TUU

    ReplyDelete
  4. Jamaani huyu Raisi, ni mzuri haijapata kutokea katika Bara hili jeusi. Na watu wake weusi mpka na miyoyo yao miyeusi, maanake hawana hata huruma kwa wanyonge, ni wakandamizaji na waoneaji kwa wanyonge hawana hata huruma, wako radhi waibe wahilimbikizie, mwisho wa siku wausudushwe na kujiona miungu watu, yaani hilo kundi la hao watu ni shidaaa kwa wengine na mustakhabali wa maendeleo ya Taifa, mwenyazi Mungu mjalie kheli na baraka raisi wetu mpendwa, anaejali masikini wanyonge wasio thaminiwa ndani ya Taifa lao

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad