Rais Magufuli Atishia Kuwatumbua JIPU Mawaziri Wawili......Wenzao Wabaki Vinywa Wazi Kikaoni

Operesheni ya kutumbua majipu ya Rais John Magufuli nusura iwaangukie Mawaziri wawili ambao  pia walikuwa  manaibu  mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Taarifa kutoka katika chanzo cha kuaminiwa zimeeleza kuwa Rais Magufuli alionesha kutoridhishwa na utendaji wa Mawaziri hao na kuwafokea mbele ya mawaziri wenzao  kwa kuwataja majina katika kikao maalum cha mawaziri kilichofanyika hivi karibuni.

"Ni mazingira ambayo mawaziri hawakuyazoea kwamba Rais anawaambia moja kwa moja kwa majina, anafoka akisema anaweza kuwafukuza wakati wowote.....

"Mawaziri wamezoea mara kwa mara wanapofanya kosa au uzembe wanaonywa kwa staili tofauti, ni kama ya kistaarabu hivi. Sasa huyu bwana mkubwa hana mchezo, aliwataja kabisa, tena mbele ya wenzao ambao walibaki vinywa wazi.

“Wewe (anataja jina la Waziri) na mwenzako (anamtaja jina pia) nitawatumbua,” Chanzo cha gazeti la Rais Mwema kinamkariri Rais Magufuli.

Mawaziri hao ambao ni wabunge wa kuchaguliwa majimboni kwa upande wa Tanzania Bara, wanaongoza wizara nyeti ambazo zinasimamia sekta mtambuka, wizara ambazo zinagusa sehemu ya ahadi za mabadiliko alizonadi Magufuli wakati akigombea urais katika kampeni za mwaka jana.

Chanzo hicho kilieleza kuwa Rais Magufuli aliwaonya pia mawaziri wengine ambao alionesha kutoridhishwa na utendaji wao kwakuwa hawaendani na kasi yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

“Magufuli alitaka atoe mfano kwa mawaziri wengine kwamba wao si watu maalum sana. Kama wanavyotumbuliwa watu wengine na wao pia wanaweza kutumbuliwa,” kiliongeza chanzo hicho

Rais Magufuli aliunda Baraza lake la Mawaziri mwishoni mwa mwaka jana na kuwashauri wasifanye sherehe ya kuteuliwa kwakuwa wakifanya vibaya hatawaonea haya atawaondoa mara moja bila kujali majina yao.

Utendaji wa Rais Magufuli umeendelea kusifiwa kila kona hususan katika kuwawajibisha viongozi wa ngazi zote na kuonesha nia ya dhati ya kuwahudumia watanzania huku akipambana na uzembe na ufisadi.

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kuna siri sasa ndani ya baraza hilo chefuuuu

    ReplyDelete
  2. TUNASHUKURU SANA MR PRESIDENTI UNATUPA RAHA WANANCHI WAZIRI KAMA KASHINDWA KUENDANA NA KASI YAKO TUMBUA TU WALISHAZOEA KULUINDWA HAO WAKATI SASA HAUPO KIZURI ZAIDI ULISHAWAELEZA ASIYEWEZA KUENDANA NA KASI YANGU AJIKATAE MAPEMA SASA KWANINI WAKULETEE ZENGWE NA WAKATI WEWE NDIO BABA. TUNASHUKURU MUNGU KUTUPATIA KIONGOZI MWENYE HOFU YA MUNGU NA MWENHYE UTHUBUTU SAFI SANA JPM TUNAFURAIA KASI YAKO WALIZOEA HAO KIONGOZI LAZIMA UWE SIRIASI NASISITIZA NCHI ILIFIKA PABAYA SANA ASANTE MAGUFULI

    ReplyDelete
  3. HII INGEINGIZWA KWENYE KATIBA INGEKUWA POA SANA

    ReplyDelete
  4. Barabara za uswahili pia ziwekwe lami sio mmeng'ang'ania fly over tu wakati barabara za kawaida haswa uswahili vumbi mtindo mmoja watu wanaathirika sana kiafya kulivuta vumbi usiku na mchana ila mitaa yenu huko Oysterbay na Masaki lami tupu mpaka barazani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwanza sura ya nchi kupeendeze reception kwanza Alafu na uani kutafwatia, tukianzia uani wala hatuto onekana kama tumependezesha, au tumepiga hatua, reception kwanza

      Delete
  5. Tumbua na maraisi waliopita na familia zao kwanza.hawa ndio chanzo cha matatizo yote.walishindwa kuongoza, waliavhia uhuru watu wafanye watakavyo, walia hia mianya, na walihusika pia kwenye biashara binafsi.ndio waliotaifisha benki, majumba, viwanda na kutoa mikataba holela kwa wawekezaji waporaji na hewa.hapo utafanikiwa kuvishika pia hivi vidagaa.hawa maraisi ndio viongoxi na majipu makuu.

    ReplyDelete
  6. Ye mwenyewe jipu na hakuna wa kumtumbua.mwizi wa kura huyoooooo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Weee nawe una lako jambo, sisi tuliowengi tunataka kiongozi mzuri kama huyu kwa mustakabali wa taifa, sio siasa au kiongozi kuatu asiejali mustakabali wa Taifa, taifa liligubikwa kwa corrupition nyingi kila kona, maendeleo yangekuwa ni ndoto tena za mchana kweupe

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad