Rais Magufuli Awagomea Wabunge Nyongeza Ya Mikopo Ya Magari

Katika kile kinachoonekana amedhamiria kuendelea kubana matumizi ya serikali, Rais John Magufuli amekataa ombi la kuongeza fedha za ununuzi wa magari kwa wabunge pamoja na fedha za mfuko wa bunge.

Baada ya kuchaguliwa, wabunge walipatiwa milioni 90  za mkopo kwa ajili ya ununuzi wa magari, lakini baadhi yao walieleza kutoridhishwa na kiasi hicho, wakidai hakitoshelezi na kutaka kiongezwe hadi sh. milioni 120.

Taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa wabunge waliwasilisha ombi kwa Rais Magufuli kuongezwa fedha lakini ombi hilo limekataliwa.

Chanzo cha kuamini kimedokeza kuwa mmoja wa wabunge wa CCM alimkumbushia Rais Magufuli ombi hilo wakati wa kikao cha chakula cha jioni, kilichofanyika wiki iliyopita mjini Dodoma.

Chanzo hicho kilieleza kuwa Rais Magufuli alikataa kuwaongezea wabunge fungu hilo kwa madai kuwa serikali yake haina fedha.

Kilieleza pia kuwa Rais Magufuli alikataa kuongeza fungu la mfuko wa jimbo kwa kuwa serikali haina fedha huku akiwataka wabunge kufanya kazi kwa bidii.

"Rais alisema kwa sasa hali si nzuri, amekumbana na changamoto mbalimbali na kutuahidi kulichukua ombi letu, endapo hali itatengemaa atatuangalia kwa sababu hata yeye analitambua hilo kwa sababu alikuwa mbunge."Kilisema chanzo hicho

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ama kweli waheshimiwa wasio ona huruma kwetu..kodi Ni zetu tunao umia Ni sisi..wao waendw Bunge Na kutoroka vikao au kuja kusinzia Kama si kulala tumeomba wasaini mahushurio eamezua hoja utumbo kkakataa kwa kujifananisha Na wanafunzi..sasa wanataka pesa zetu Ili anunue shangingi atorike vizuei vikao..ukitaka kujua ealivyo koda dhana za uzalendo Na kujali maslahi binafsi kumbuka mh. K Majaliwa alipo lets suala/Hoja ya pikipiki Na Bajaji hii Ni igizo tosha kwa awamu yetu Ni ya kubana matumizi..ameizungumzia wapi? BUNGENI KWA KINA NANI..WABUNGE..JE HAMUELEWI!!!! MNATHUBUTU KUMKABILI JPJM...MMEBUGI STEP HII NI TEAM YA MAENDELEO YA NCHI HAPA KAZI..TUONEANE HURUMA NA TUTAFAKARI. KABLA YA NYINYII KUTUUMIZA SISI MA MJITOE MUHANGA KABLA YETU SISI. HAPO NTATUPA IMANI

    ReplyDelete
  2. Eti Nini???? Mikopo na nchi iko katika michakato ya ukusanyaji Kodi and utumbuaji Majipu kwa ajili ya maendeleo ya nchi.. na hawa ndugu zetu wakosa nidhamu bungeni wanataka matumizi zaidi juu ya kutuumiza na posho zao ambazo baadhi yaohawawajibiki nazo bungeni ... hatujapagawa wala JPJM na Kassim Majaliwa waridhike nalo hili..Tunataka kuona Huduma muhimu kwanza zinawafikia Wananchi au mmesahau kuwa mko katika awamu ya TANO...ikiongozwa na Mwanetu JPJM akisaidiwa na Timu kabambe ya MAbadiliko ya Huduma kwa Mtanzania... Na hiyo Huduma kwea taarifa yenu imfate mwanchi na si kinyume kama ilivyo kuwa awali Mwanchi anazungushwa nenda rudi kuitafuta Huduma... Juzi naibu waziri Mavunde kapewa Maji wanayokunya wananchi... Amejitolea kuanza kufanya kazi ya maji safi kwa pesa Zake... Huu ni Mfano wa kuigwa... Ulibaho W
    Mwahaaa.... Hapa ni Kazi Tuu.... Amini usiamini Hatuto angushwa... WACHENI KUOMBA YASIYO WEZEKANA AU KUKUBALIKA.. NIA NA DHAMIRA IKO WAZI... MATUMIZI TUNAYABANA,, SAFARI ZISIZO NA FAIDA TUMEZIFUNGIA... SHEREHE ZA KITAIFA BADALA YA KUPOTEZA PESA TUNAFANYA USAFI KWA FAIDA YETU NA JAMII... LEO MNATHUBUTU KUONBA PESA ZAIDI... ZAIDI...ZA NINI KAMA NI KWAMBA HAMUELEWI KINACHOENDELEA... INASIKITISHA TENA SANA...TUWE WAZALENDO TENA YENYE HURUMA KWA WALIPA KODI JAMANI...JP TUNAKUAOMBA CHONDE CHONDE...TUWAFANYIE MWAMKO WA AWAMU YETU KUHUSU ROAD MAP TO ATTAIN THE GOALS....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wadau hapo juu..nakubaliana nanyi..hawa so selfish. Wengi Wao wako holidei Dodoma. Wanasahau kilicho wapeleka..mpaka wanabuni mwongezeko WA mkopo..mkopo...mkopo..JP anakazi kubwa ya kufundisha Na kuelimisha Ili aeleweke ....

      Delete
  3. Nashindwa Kuelewa Vigezo vipi vimeweza kuwapa Uwezekano wa Kupata kura na kuwakilisha majimbo ya wananchi.. Itabidi tubadilishe labda mfumo mzima wa elimu...
    Inawezekana wapiga soga na kubwabwajika katika vitongoju vyao vinawapa KIKI ya kuwa Mbunge.. Lazima wafanyiwe Tathmini upya na kuwapa mwamko wa wajibu wao Bungeni... Mil 90 mimi nikienda kuomba mkopo ntafukuziwa mlangoni... Hawa ndugu zetu wanaona ndogo wanataka Mil 120????? Mhhhhhhh....Hivyo Benki gani wana draw....Ndugai Upo hapo!! Mimi niko Tayari Kuwaelimisha hali halisi ya taifa letu ambao wao wawakilishi wet Hawaijui. Hivi tutakwenda kweli.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau umenitachi tena Sana..ndiyo nchi yetu Na tamaa bado zinaendelea wangoja mwanya tuu akipata hawachi si anajua atamaliza muda wake asipofanya kweli sasa lini atafanya kweli..JP NA MAJALIWA TUMEWAPA MZIGO MKUBWA WA HAJUKUMU MANAKE HII NDIYO HALI HALISI WALIYOIKUTA NA WANAPAMBANA NAYO..JP MUNGU AKULINDE KAZI NA CHANGAMOTO ZIKO PANDE ZOTE..UTUMUSHI / uwajibikaji / UELEWAJI WA MWENDO NA MAJUKUMU..NK

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad